Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani askari Polisi, Pacificius
Cleophace Simoni, kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mwanahabari
Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha
Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa
Kwa mara ya kwanza Simoni alifikishwa mahakamani hapo Septemba 12
mwaka 2012 akituhumiwa kufanya kwa kukusudia mauaji hayo wakati
mwandishi huyo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari
kwenye ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri
umeilazimisha mahakama hiyo chini ya Jaji Kihwelo kuibadili kesi hiyo
kutoka kwenye mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya bila kukusudia
ambayo hukumu yake ameisogeza mbele hadi kesho Jumatano.
Baada ya mabadiliko hayo, wakili wa upande wa Jamhuri, Adolph
Maganga, aliiomba mahakama hiyo imhukumu mtuhumiwa huyo kifungo cha
maisha jela kwa mujibu wa Kifungu cha 198 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu
huku wakili wa utetezi, Lwezaula Kaijage akiiomba mahakama hiyo
impunguzie adhabu kwa kumfunga kifungo cha nje.
0 Comments