Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya kati ya yalioandikwa ni huu utafiti kwenye gazeti la Mtanzania wenye kichwa ‘Chips chakula hatari’.
Ulaji wa chipsi umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo la damu kisukari na saratani za aina zote. Imeeleza kuwa sahani moja ya chips kavu huwa na mafuta yanayokaribia nusu kikombe cha chai ambayo ni sawa na ujazo wa milimita 250.
Hayo yalisemwa na Mtaalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ulumbi Kilimba alipokua akizungumza na gazeti la Mtanzania ambapo alisema walaji wengi wa chipsi wako kwenye hatari ya kutengeneza sumu kwenye miili yao bila kujijua.
Alisema jambo la kusikitisha ni kwamba wafanyabiashara wengi wamekuwa hawazingatii umuhimu wa kutumia mafuta mara moja katika kukaanga vitu hivyo.
Utafiti wa Marekani nao pia umeeleza kwamba ulaji wa mara kwa mara wa chips unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito. Sababu ya wanga ulio katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000
0 Comments