Roma,zimbabwe ,video with lyrics





Wengi mlijiuliza walionteka ni maaskari?



Mkanitafuta vituo vyote central hadi stakishari
Wakasema… hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari
Dah
Ya caisar mwachie caiser
Machozi yenu yatalipwa me nafunga na kusali
IMBA ROMA IMBA X3
Mungu wa Paulo… ndio mungu wa daudi
Na ndio mungu wa john mnayemuita yohana wa yahudi
Mwanangu alimuuliza,mama baba lini atarudi?
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sinabudi
Fahamu yakuwa
Me sio tu rappa pia ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo biblia
Kipi bora?
nife museme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa… ila nnawaachaje waliobaki?
Nani katiyenu mwanangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji?
Wapi atapata mapenzi?
Mama nae
Wapi atapata mahitaj na malezi?
Na report ya upelelezi
Vipi akiteka mtekaji?
Je… kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja kuniona
Mnangoja mje msibani?
Nlipokuwepo skuwa nnajua hii saa nne hii saa nane
Nlichohitaji… nitoke mzima na ndugu zangu tuonane
Nimechapwa mijeledi
Nimevunjwa bila huruma
Ahsante mliopaza sauti
Nimeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefumbwa macho
Mikono nimefungwa nyuma


NAKWENDAA ZIMbABWE ZIMAMA YELELE MAMA WEE X4
IMBA ROMA IMBAA
SEMA BABA WEEEE

Nasimama na nnaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linaoza msoga kibiti linaoza shamba
Walioniteka hawakuja na noah… ni uvumi na visanga
Ila KUTEKANATEKANA
Ni uhuni wa kishamba…
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu ni kuijenga Tanzania moja
Me skuona 
nyota kwa shoulder ila najua we ni soja
Inshaalah
Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order? Ewalah
Aminini siku hazigandi
We ni yanga me ni samba kuwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani
Samba akichukua kombe sijui atapona nani?
Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa mungu…namshtakia aliye juu
Kwanza lini?
Na kwanini?
Me nimtukane 
mjomba?
Umepewa gari ya wagonjwa mitaani unanijengea bomba
Me mbarikiwa na nikifa kuume kwa baba ntaketi
Na mtu wa watu.. that’s why lilisimama bunge la
bajeti
Kunijadili mtanzania kuwa MAKINI PIA MAKINIKIA
NAYATUNGIA MAPINI PIA
Me nlitabiri utakuwa rais kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahis ila pongezi unastahili
Waliosadiki roma ataonekana kabla ya jumapili
God bless imetimia injili niliyoitabiri

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMAMA YELELE MAMA WEE X4
IMBA ROMA IMBAA
SEMA BABA WEEEE

Post a Comment

0 Comments