Yusuph Manji amkataa Wakili Kibatala kusimamia kesi yake

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na Mfanyabiashara, Yusuf Manji baada ya kukubaliana na pingamizi zilizowasilishwa na DPP.

hata hivyo kabla ya kutupiliwa maombi hayo, Manji alisimama na kuieleza mahakama kukataa kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa sababu za kisiasa.

Manji amedai, alipopeleka maombi ya dhamana mahakamani hapo, alimpa maelekezo wakili Joseph Tedayo lakini alishangaa kesi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kisikilizwa maombi yake aliwakilishwa na wakili Peter Kibatala.



Post a Comment

0 Comments