KAZI ZA WASANII ZINAPOTEA KWA KUKOSA UHIFADHI MZURI WILAYANI SONGEA

Tatizo la wasanii wengi nchini Tanzania na hata ndani ya mkoa wa Ruvuma ni pale wasanii wachanga na wasio na jina kubwa wanaposhindwa kuhifadhi kazi zao katika sehemu salama itakayowasaidia kupata kazi zao hata baada ya miaka mingi ijayo
sehemu hizo ni kama kwenye blogs,websites na hata katika hifadhi za email zao kama google drive na dropbox

Imeonekana wasanii wengi wilayani Songea hawana uhifadhi mzuri wa kazi zao na kusababisha tatizo la kupotea kwa kazi hizo

"Nimepoteza nyimbo zangu nyingi sana na nyimbo zingine nilibahatika kufanya na wasanii wakubwa na producers wakubwa ila zimepotea na siwez kuzipata tena kwa mfano nilitoa nyimbo inaitwa bonyeza ok.... producer pfunk ft jnature na kr mwaka 2007
Nyimbo nyingine ni njoo tena ambayo nilifanya chini ya producer said komorie ila nilibahatika kuipata mbali sana kuna mtu alinihifadhia"

Alisema Hamis Rashid A.K.A H.R ambaye ni msanii wa muziki wa bongo flavour mkoani Ruvuma

"Ni kweli wasanii wa Ruvuma na hata nje ya ruvuma wanakumbana na tatizo la uhifadhi wa kazi zao na kuna wasanii wengi tu wamefuata kazi zao hapa ambazo wamezifanya muda mrefu zaidi ya miaka mi 5 lakini bahati mbaya ni vigumu kuzipata kwasababu hivi vyombo vinahitaji marekebisho kila baada ya muda na wengine wanafikia hatua hata ya kurudia kazi zao'' ....
mr paul producer wa wisher record....

Huwa tunawashauri wasanii wengi kuhifadhi kazi zao katika mitandao na si kumtegemea producer au kutumia mifumo dhaifu kama flash...memoricard na cd ambazo ni rahis sana kuharibika na lawama kubwa kutoka kwao ni gharama ya kuingiza kazi zao kwenye mtandao alisema producer mr paul

Ajuco times ilipata bahati ya kuongea na afisa tamaduni bwana Andrew Mwafwalo na kuthibitisha uwepo wa tatizo hilo kwa kutambua tu lakini hajapata malalamiko na ameomba kama kuna wataalam wawaaaidie wasanii wa mkoa wa ruvuma kuhifadhi au kuwatengenezea sehem nzuri itakayowasaidia kuhifadhi kazi zao

Post a Comment

0 Comments