Rais Robert Mugabe ameondolewa Madarakani rasmi na Chama chake cha Zanu Pf

Rais Robert Mugabe ameondolewa Madarakani rasmi na Chama chake cha Zanu Pf na makamu wake aliyefukuzwa wiki iliyopita kupewa madaraka kuongoza chama hicho.Katika mkutano wa Kamati kuu ya Chama hicho uliofanyika mda mfupi uliopita jijini Harare umemuondoa mke wa Rais Mugabe bi Grace Mugabe kwenye chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuhusika katika kukivuruga chama hicho.Mda mfupi uliopita mwandishi wa Bbc  Andrew Harding akiwa katika mkutano huo ametuma video Kwenye ukurasa wake wa twitta akionyesha wajumbe wa kikao hicho wakisherehekea baada ya kiongozi huyo kuondolewa.Taarifa kutoka mkutanoni zinaeleza kwamba baada ya hatua hiyo chama hicho kitaandaa utaratibu wa kumuondoa Mugabe kwenye nafasi ya Urais wa nchi hiyo

Post a Comment

0 Comments