Mziki &Media (Ugomvi,Makundi)

Na ElnandoHumphrey

Mziki mzuri upo bongo aisee. Wasanii wa Tanzania wameushika mziki kwa kila aina ya muondoko. Ukitaka Hip Hip Tanzania wapo wasanii wengi na mahiri katika muondoko huu wa hip hop. Na mziki kama RNB, BOLINGO etc. Kakaangu Nchakalih anasema hawaelewi wanaijeria, na sio wakali bhana anashangaa ni kivipi wanatawala game la Afrika. Labda promo na kupendana wenyewe kwa wenyewe.
Miaka ya 90 mziki ulikolea sana na kabla wasanii kama kina Duly Syks kuibadili hip hop na kua bongo flavor wapo na yapo makundi yalitamba katika kutoa burudani nzuri ya mziki wa Hip Hop. Kundi kama kwanza Unit ambalo lilikua na wasanii kama Chief Rhymes (zavara) , KBC (KIBACHA) Adili kumbuka (RIP) , Zomba (RIP) na wengine wengi. Msanii mmoja mmoja kama Sugu .jabir saleh etc
Mziki ulikua makundi na wapo waliosonga kivyao na wakahit. Kipindi hiko media zilikua ni wasikilizishaji wa ngoma hizo japo ilikua kwa uchache mno ila walisikika. Hadi miaka ya 2000 mziki ulichanganya mno
Makundi kama HBC (hardblasters crew) kundi likiongozwa na Professor J , TMK wazee wa mapanga , Kikosi cha mizinga, Nako2nako na makundi meengi yalitamba sana kipindi hiki lakini yalitamba kupitia media sasa.
Clouds fm wazee wa mawingu wakaibuka na kuushika mziki wa bongo kisawasawa. Wengi walilalamika kubaniwa aisee na wasanii baadhi waliungana kupinga uonevu uliofanywa na kituo hiki cha Radio ambacho kilijikita katika burudan.
Makundi ya mziki yalianza kushikwa na watu. Walioshika makundi hayo wakaanza kupata nafasi katika media. Namaanisha mziki wako huwez pigwa bila kuwa karibu na manager flani au kuwa mtu wa kundi flani
Real hip hop is not on the radio... is on the street. Wapo walioikacha radio na kuzamia ulaya na wapo waliokomaa na game la bongo kibish bish wakiamini watapasua siku moja. Wengi walikuwepo sasa hivi wako wapiiii? Anauliza balozi.
Kundi la TMK likiwa chini ya Said Fella na Kundi la tip top likiwa chini ya Abdul Bonge (RIP) huyu alikua kaka wa BAbu Tale. Ilisadikika , naomba nieleweke vizuri ... ILISADIKIKA YA KWAMBA ili mziki wako uweze kurushwa kwenye radio ni lazma uwe na ushkaj na hawa jamaa. Kama hauna ushkaji nigga Bounce.
Kinachoitwa unyonyaji kikatokea
mameneja wakawanyonya wasanii na makundi yakavunjika.Walisema wenyewe wasanii sio mimi jamani. TMK ilivunjika ikapata TMK halis. Umegombana na Fella utaskika wapi?? Wengine wakakomaa na TMK og mpaka mwisho japo kujitoa hakukwisha. Mara leo katoka mara karudi mara huyu kapotea hawa wawili wanapendelewa hawa wanabaniwa. Alafu unazima kama taa.
Baadhi waliungana kupinga uonevu huu... Sugu akaungana na wenzake kama Rama Dee... Dany msimamo..Maujanja saplayaz (mapacha),SogyDogy hunter mzee wa kibanda cha simu na wengine weeengi na kuanzisha harakati za AUNTVIRUS kwa dhumun la kukichafua na kupinga uonevu huo kwakua hawakua na pa kulalamika zaid ya kutumia mziki wao kuwachana wazinguaji.
Waliishia kupatana japo kinafki (kama nimetumia neno baya samahanini). Ila issue ikaisha kimya kimya japo Auntvirus walitishia amani sjui hata walikwama wapi
Wakaibuka wasanii wengine katika kipindi ambacho mziki umekua ukilipa haswa
TAZAMA KWA MAKINI KILICHOENDA KUTOKEA
Msanii mwenye nguvu kama Diamond akapata management ile ile iliyotikisa zamani chini ya Babu Tale AKA Babu talent kama anavyomtaja nikki mbish sjui kwanini jamaa aliimba hii nyimbo ila tukumbuke ni washkaji now. Roma akasema boss kamganda dangote kaisahau tip top hahahaa yani kaacha kundi kamfwata mchizi..tuache hilo.
Diamond Akajitahid kupata mpenyo wa umaarufu akapata na hela alafu ghafla yeye na managements rafiki yani Tale na Fella wakaigeuka clouds na kuanzisha vitu vyao (wasafi media) ilitangulia tv na radio ikafwata. Japo wengine wanasema kuna mikono ya wasaliti, mara hii ni ya mke wangu ila raia tunamjua Diamond bhana ndo anamiliki hivi vituo.
Upinzani mkubwa umetokea na sijui mwokovu ni nani? Tale na Fela wameokoka na kuungana na wasanii au clouds imeokoka kujitoa kwa Managers hawa wawili. Kupitia maoni yao tutapata kuskia nani alikua mnyonyaji kwakua watazamaj hawana majibu zaidi ya kuskiliza wahusika wanasemaje.Hili ndio game la bongo bhana

Post a Comment

1 Comments

  1. Safi kamanda, umeelezea vyema Ingawaje Kuna nakisi kimtindo ila fresh..
    Mwanaharamu hapa

    ReplyDelete