Utashangaa Kuona Jinsi Majivu ya Tupac Yalivyotumika

Kuna hadithi tatu zinazozunguka juu ya kile kilichotokea kwa majivu ya Tupac, kama hautambui ni kwamba, Baada ya kifo cha Tupac alichomwa moto ikiwa kama destruri ya watu wengi. kupenda kufanyiwa hivyo au hata familia kuamua.


Simulizi Mbili zinaaminika kabisa na ya mwisho ina ukakasi kidogo.

Wacha tuanze na hii yenye mashaka kidogo.

Kikundi cha mziki cha Tupac kinachojulikana kama OUTLAW wanadai walichanganya majivu ya tupac na sigara ( sijui ni sigara kubwa au ndogo) na kuyavuta. Lakini hakuna mwanachama wa kikundi anayeonekana kukubaliana ni wakati gani na mahali ambapo waliyavuta majivu hayo. Hii inaleta ukakasi kuamini kama ni kweli walifanya hivyo . Kwenye nyimbo yao kikundi cha OUTLAWS inayojulikana kama Black Jesus, dakika ya 2 sekunde ya 15 tupac anatoa husia kwa rafki zake kuwa baada ya kifo achomwe moto na majivu yake yavutwe kama sigara.


Hiyo story imekaa juu juu sana, japo kuna wanaoamini kuwa ni kweli walichanganya majivu yake na vileo mbalimbali na kuvuta. Kwa chanzo cha kuaminika zaidi, mama wa Tupac ambaye naye ni marehemu, Afeni Shakur. Siku moja baada ya Tupac kufariki, alichomwa moto, na kukabidhiwa majivu yake. 

 
Baadae Afeni alisema kwamba alieneza majivu ya mwanaye mahali Fulani huko Los Angeles na pia alichukua majivu yaliyobaki na kurudi nayo nyumbani kwake huko Stone Mountain, Georgia. Na huko alieneza majivu yaliyobaki katika bustani yake.


Simulizi ya tatu kwa mara nyingine inatoka kwa mama wa Tupac Afeni Shakur. Na simulizi hii inahusiana na kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Tupac, mnamo 2006. Ni kwamba Afeni Shakur alichukua majivu ya mtoto wake na kwenda nayo Soweto huko Afrika Kusini.


kulingana na maelezo yake SOWETO S.A ndio "MAHALI WALIPOZALIWA BABU ZAKE KI HISTORIA". Pia anasema Soweto ndio mahali yalipozaliwa mapigano ya demokrasia na kupinga ubaguzi wa rangi yaani Apartheid, mfumo wa kikatili ambao ulitekelezwa na makaburu huko South Afrika", Afeni alishawishika na tabia ya mwanae Tupac ya kusimama imara kama mtetezi wa haki za watu weusi. Kuna mipango mingine inayohusiana na ziara ya Afeni nchini Afrika Kusini, kama vile ujenzi wa makumbusho huko Soweto kwa kuheshimu mziki na harakati za Tupac, ambayo itakua ni sehemu ya jumba la kumbukumbu ya muziki na sanaa nchini Afrika Kusini. Alisema: "Matukio yaliyotokea [Soweto] ni sehemu ya historia yetu na itakuwa heshima kwa mwanangu kupumzika mahali hapa maalum".

Post a Comment

0 Comments