Historia Ya Mwanamuziki Marvin Gaye










Marvin
Gaye mtoto wa pili kati ya watoto wanne kwa Mchungaji Marvin Pentz Gay Sr na
mwalimu Alberta Williams. Baba yake Marvin alihubiri katika kikundi cha Kanisa
la sabato kinachoitwa “HOUSE OF GOD” Nyumba ya Mungu,
Wakiwa na kanuni
madhubuti
zenye maadili na mafundisho yenye mchanganyiko "Uyahudi wa Orthodox na harakati za watu weusi" hawa hawakuwa
na sikukuu wala sherehe ya siku ya kuzaliwa. Baba wa Marvin alikuwa baba
anayeogopeka nyumbani kwake, alikua mkali na hakusita kugawa dozi kwa watoto
wake wanne pale wanapozingua (kuwachapa
kisawasawa)
.
Jeanne
Gay alisema kuwa baba yao hakuwahi kuelewana na Marvin.
Lakini kumbuka,
Hata uwe mkali vipi, kuna mtoto utamshindwa tu na ataishi anavyotaka. Marvin
aliacha shule na kujiunga na Jeshi la Anga la Marekani. Aliacha kazi baada ya
miezi kadhaa tu kwakua alikataa kufuata masharti ya mkuu wa kikosi (ODA).
Ndugu
yake Frank akaungana na kaka yake katika shughuli ya muziki na kuanza kurekodi
huko Motown (Marvin aliwahi kuwa mpiga ngoma kabla hajawa muimbaji kamili)
Alibadilisha
jina lake kutoka Marvin Gay kuwa Marvin Gaye na kuongeza 'e' ili kujitenga na
baba yake (Alitengeneza jina la ukoo wake) pia alidhamiria kumaliza mgogoro
kuhusu ujinsia wake kwakua jina Gay linamaanisha mtu mwenye mahusiano ya jinsia
moja (kiuhalisia Marvin hakuwa mtu wa hivyo, bali ni jina tu la Baba yake),
alimuiga rolemodel wake Sam Cooke, ambaye pia akaongeza 'e' kwa jina lake la
mwisho.
Marvin
alioa mara mbili. Ndoa yake ya kwanza ilikua na Anna Gordy dada wa Berry Gordy,
mwanzilishi wa Motown record
label
. Aliwahi kumuimbia vibao kama “Stubborn Kind of Fellow” na " You Are a Wonderful, walimlea Marvin Pentz Gaye III (Juni 8, 1965). Mwaka
1973 alipotoa album ya Let's Get It On akaanza kutembea na mtoto wa Slim
Gaillard aliyeitwa Jan Hunter na kupelekea kutengana na Anna. Wawili hao
walifanikiwa kupata watoto wawili Nona Marvisa Gaye (Septemba 4, 1974) na
Frankie Christian Gaye ( Novemba 16, 1975).
Walioana
Oktoba 1977 pale ndoa ya Marvin na Anna ilipovunjwa rasmi. Walitengana kwa sababu
ya mvutano na mwishowe walipeana talaka mnamo Februari 1981.
Hapa
Marvin akaingia kwenye msongo wa mawazo na kutumia madawa ya kulevya. Mwisho
aliamua kurudi nyumbani kwao mwaka 1983. Asubuhi ya April 1, 1984, kulikua na
malumbano kati ya baba yake Marvin (Marvin Gay, Sr) na mke wake Alberta. Kama
unavyotambua baba yake alikua mtata sana na haambiliki, Marvin akaamua
kumsaidia mama yake kwa kumgomea baba yake kuwa LEO UKIENDELEA KUMUONEA MAMA LAZIMA TUTAPIGANA. Baba wa Marvin
akachukua bastola na kumpiga Marvin kifuani upande wa kushoto (kwenye moyo).
Mdogo wake Marvin ambaye pia alikua mwanamziki,
alikua jirani na maeneo hayo na ndiye aliyesikia maneno ya mwisho ya Marvin,
alisema “Nimepata nilichokihitaji, nilishinwa kujiua mwenyewe na leo nimemfanya
aweze kuniua”
Kumbuka Marvin aliwahi kujaribu kujiua Mara tatu.
Mwaka 1969 alitaka kujipiga bastola, wakamzuia na Berry Gordy. Baada ya miaka
10 alijaribu kuji overdose na madawa ya kulevya lakini hakufa, Siku kadhaa
kabla hajauawa na baba yake, alijirusha kwenye gari lililokua kwenye mwendo
mkali na hakufa.
Kwa maelezo ya baba mzazi wa Marvin akiwa mahabusu
alisema “hakudhamiria kumpiga risasi mwanaye, siku hivyo Marvin alikua kama
mbogo na alimshambulia kwa ngumi nyingi. Alipojaribu kukimbilia chumbani kwake,
Marvin alimfwata. Alimwogopa kwasababu alikua anatumia madawa aina ya cocain na
kuhisi angemdhuru. Hata wakati anapiga risasi hakujielewa na alidhani kulikua
na baruti tu ambayo ingemtisha Marvin.

Post a Comment

0 Comments