Ugonjwa wa kucheka, Pseudobulbar Affect, / PBA Kwa walioitazama na wasioitazama Movie ya Joker tujuzane hili

Joker au jokeri, wacheza karata wanampenda na wanamwogopa, akikulalia huyu unahesabiwa una 50, kwenye adhabu unamlambisha mtu 5. Tuachane na huyu

Joker anayejulikana kwa jina la Arthur Fleck (jina halisi Joaquin Phoenix) kupitia movie ya JOKER 2019 na movie zingine nyingi zinazomuonyesha kuwa mpinzani mkubwa wa Batman kwa miaka 80 sasa tunasimuliwa stori zake.
Flexk anaonekana kupambana na ugonjwa wa akili, ugonjwa unaomfanya asipendwe na kila mtu. Kihistoria anaonekana anabaguliwa toka akiwa mdogo mpaka anakua mtu mzima. Ana ugonjwa wa kucheka, yani jamaa anaweza kucheka hadi akatokwa na machozi,
mpaka alikua anatembea na karatasi ili akianza kucheka anakupatia mtu wa karibu yake usije kumwona mdwanzi. Kikaratasi kinakuambia samahani, nina ugonjwa wa kucheka naomba unisamehe, hapo hata kukuambia kwa mdomo anakua hawezi

Movie ya JOKER haikusema ni ugonjwa gani Fleck alikua anaumwa, lakini kitaalamu wanasema huu ugonjwa wa kushinwa kujizuia kucheka unaitwa Pseudobulbar Affect kwa kifupi PBA Hali hiyo husababisha kucheka kicheko kisichoweza kudhibitiwa au hata kulia,
na kawaida hutokea kwa watu ambao wana Multiple sclerosis (MS) na amyotrophic lateral sclerosis (ALS) (matatizo katika neva au majeraha kwenye ubongo) Wataalam wa afya watatusaidia kwenye hili

 

Phoenix AKA Fleck aliwahi kusema, nafasi aliyoicheza amewawakilisha wale wote wanao/waliochekwa wakiwa mashuleni, mitaani- kwaajili tu ya kuwa tofauti na watu wengine (Mwonekano, ulemavu) na kukosa sehemu ya kufikisha matatizo yao. Kisaikolojia inaweza mfanya mtu kuwa mhalifu.

Post a Comment

0 Comments