JINSI LUGHA YA KILATIN ILIVYOKUFA

Kwasasa imekua lugha inayotumika kwenye mambo maalumu tu, je kuna ubaya nikisema hii lugha imekufa?, kama ulikua hujui kuwa lugha inakufa ndo ujue leo, wataalam wa lugha wanaweza kuelezea lugha inakufa vipi.

kama ni mfuatiliaji mzuri wa historia, najua haukuwepo ila unatambua jinsi utawala wa warumi ulivyokua na nguvu kabla hata ya ujio wa yesu, enzi za kina kaisari na Cleopatra. Nikukumbushe tu Malkia Ckeopatra wa Egypt alimzidi yesu miaka 69
Lugha yao ilikua kilatini. Baba wa ufalme wa roma alikua Romulus na iliyemfia Roma aliitwa Romulus Augustus, tawala ilijengwa na kubomolewa na Romulus (unampatia mtoto jina kudhani atakuwa na bahati kama mwenye jina, kumbe ni nuksi tupu). Sitambui ni kitu gani hasa kilipelekea utawala wa waroma kuanguka na hiyo haikua sababu ya lugha ya kilatini kupotea kwasababu ilizidi kuwa hai zaidi ya miaka 500
karne ya 5 baada ya kuzaliwa Yesu, roma ilishikwa na wajerumani. Wavamizi zaidi ya makabila ma 5 ya kijerumani yaliishika Roma kinguvu. Kila kabila lilizungumza Lugha yake. Chakushangaza baada ya muda fulani, wavamizi wote walikua wanazungumza kilatini. Bwana awe nanyi

Mimi na wewe tujiulize, je lugha mama (kingereza Orijino kabisa, kwasasa sidhani kama kina mzungumzaji) ambacho kimezaa lahaja mbalimbali tena nyingi na chenyewe kubadilika kwa misamiati mipya ndio kufa huko?
Tofauti ya kilatini na kingereza ni kwamba, karne ya 6 baada ya utawala wa warumi kuanguka ndipo lugha hii ilianza kupata kashikashi. Lahaja mbalimbali ziliibuka na kuchota lugha ya kilatini, lahaja hizo za warumi zilikua ni Kifaransa, kireno, kiitaliano, kispanish (kihispaniola) na kiromania. Kiitaliano na kiromania hufanana kwa kiasi kikubwa na hivyo wazungumzaji wanaweza kuelewana. Japo lugha hizo zote 5 zinaingiliana kidogo. Wenyewe huziita lahaja za kirumi (romance language / dialects)
Hivyo watu waliacha kabisa kuandika na kutumia kilatini na kuanza kucheza na lugha hizo tano. Hivyo kusema kilatini kimekufa ni sawa na kusema kingereza halisi kimekufa kwakua hakina mzungumzaji. Japo ni ngumu kukiita kilatini kiitaliano cha zamani loooh mambo haya si mchezo, kilatini huitwa hivyo hivyo latin.

Tunasema kilatini kimekufa, lakini kwanini kimekuwepo kwa muda mrefu hivi? watu wanajifunza kilatini hadi leo hii
Kulitokea dini ndogo ambayo ilitukanwa sana, na watu wa pembeni waliita dini ya mungu maskini. Maadui wa dini hii waliita dini ya kikristo (christianity) japo wenyewe walijiita KANISA (ECCLESIA). Wakristo wa kwanza walikua wayahudi na kanisa lilianzia kwenye masinagogi (nyumba ya ibada) wakiwa wanasambaza ujumbe wa ukombozi kwa ulimwengu. Wakati utawala wa roma unaanguka, dini ya kikristo ndipo ilipokua inazidi kupata nguvu. Kumbuka roma ilianguka karne ya 5. Ila hadi kufika karne ya 6 hima iliyodondoka ilikua na wakristo wa kutosha. Hadi kufikia karne ya 7, dini hii ilishaanza kuenea kwenye maeneo mbalimbali.


Jerome ambaye inasemekana alikua padri wakati huo alikua anazungumza sana kilatin, kigiriki na kihebrania, alipewa kazi ya kuchapisha biblia na Papa Damasus mwishoni mwa karne ya 4 kabla roma haijaanguka. Kwa miongo miwili huu ndio ulikua mkakati mkubwa wa kanisa. Japo chapisho la Jerome halikua chapisho la kwanza la kilatin, yalikua mengi na yalisambaa sehemu nyingi. Kwakua wakristo ni watu wa vitabu, lugha ya kilatin ilienea kabla hawajaanza kutafsiri lugha hiyo kwenda kwenye lugha mbalimbali za watawala wapya. Gothic (jamii ya watu Fulani ya wajerumani ambao ndio wavamizi wa mwanzoni huko Roma) walikua watu wa mwanzo mwanzo kutafsiri biblia kwenda kwenye lugha yao.
Ndio maana Lugha ya kilatini ni lugha official inayotumika kwenye kanisa la Roma. Ukitembelea Mji wa Vatikan, utaona bado wakatoliki wanachapisha nakala zao kwa lugha ya kilatin.



kutokea na kukua kwa dini ya kikristu ni chanzo cha lugha ya kilatini kutumika kwenye mambo kadhaa mpaka leo hii. Baadhi wanajifunza na mafunzo kadhaa ambayo ni mazuri (sayansi etc) yapo katika lugha ya kilatin.
Je lugha inaweza kufufuka? na kuwa imara upya?? na kupata wazungumzaji ambao watakua watumiaji wa kwanza wa lugha hiyo (lugha mama)??

Post a Comment

0 Comments