aliyekiitwa yesu ni nani?

Swali: "Yesu kristo ni nani?"
Jibu: Yesu kristo ni nani? Watu wachache sana
huuliza kama Yesu kristo alikuweko.
Inakubalika kikamilifu kuwa Yesu alikuwa ni
mtu aliyetembea juu ya ardhi huko Israeli
karibu miaka 2000 iliyopita. Mjadala huzuka
wakati wa utambuzi kamili wa Yesu kristo
unapojadiliwa. Karibu kila dini kubwa humtaja
Yesu kama nabii, mwalimu mwema au mcha
mungu. Tatizo ni kuwa Biblia inatuambia ya
kuwa Yesu alikuwa zaidi ya nabii, mwalimu
mwema au mcha mungu.
C.S. Lewis, katika kitabu chake kiitwacho
ukristo wa kijinsia tu aeleza yafuatayo: “nipo
hapa kuzuia yeyote asemaye upumbavu kama
wengine wao juu ya Yesu kristo. Wao husema,
“Niko tayari kumkubali Yesu kama mwalimu wa
uadilifu tu lakini sikubali madai yake ya kuwa
ni Mungu”. Hili jambo moja lapo ambalo
tusiliseme. Mtu aliyekuwa mwanadamu wa
kawaida na kuweza kusema yale Yesu alisema
bila shaka angekuwa mwendawazimu ama ibilisi
wa kuzimu. Lazima ufanye uamuzi kamili.
Uamue kama Yesu alikuwa mwana wa Mungu au
mwendawazimu. Unaweza kumtusi, kumtemea
mate na hata kumdharau. Hakutuachia nafasi
ya kumuamulia Yeye kuwa ni nani.
Je, Yesu alisema yeye ni nani? Je, biblia
inatuambia alikuwa nani? Kwanza tutazame
maneno ya Yesu kutoka Yohana 10:30, “Mimi
na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa
juu juu, hapa hakuna taswira ya kuwa yeye pia
ni Mungu. Lakini ukitazama majibizano ya
wayahudi dhidi ya maneno yake, “Hatukupigi
mawe kwa sababu nyinginezo ila kwa hili,
kukufuru. Wewe ni mwanadamu tu lakini
unajifanya sawa na Mungu” (Yohana 10:33).
Wayahudi walielewa usemi wake Yesu
ulimaanisha kuwa yeye ni Mungu. Katika andiko
lifuatalo Yesu hakuwasahihisha kwa kusema, “si
kuleta madai ya kuwa ni Mungu.” Ina maana
ya kuwa Yesu alikuwa akisema kuwa yeye ni
Mungu kwa msemo huwo, “Mimi na Baba yangu
ni mmoja.” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni
mfano mwengine. Yesu alisema, “Amini, Amini
nawaambia, kabla Abraham kuweko
Nilikuwako.” Hali iliyowasukuma wayahudi
kushika mawe iliwampige nayo Yesu (Yohana
8:59). Yesu kutangaza kitambulisho chake
kama, “Mimi ndimi” ambalo ni jina lilitumika
sana kumaanisha Mungu katika Agano la kale
ni ishara kuwa ni Mungu (Kutoka 3:14). Kwa
nini wayahudi walitaka kumpiga mawe kama
hakuwa amesema kitu ambacho kwao ni kufuru,
madai ya Yesu kuwa ni Mungu?
Yohana 1:1 yasema, “na Neno alikuwa Mungu”.
Yohana 1:14 yasema, “ na neno akafanyika
mwili”. Hii ina maana ya kuwa Yesu ni Mungu
katika mwili. Tomaso, mwanafunzi wa Yesu
alisema, “Bwana wangu na Mungu
wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi.
Mtume Paulo amtaja kama, “… Mungu wetu
mkuu na mwokozi Yesu kristo” (Tito 2:13).
Mtume petro asema, “Mungu wetu na mwokozi
Yesu kristo” (Petro wa pili 1:1). Mungu Baba ni
shahidi wa kuthibitika kwa Yesu Kristo, “Na kwa
ajili ya mwana asema, “Kiti chako cha enzi,
wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na
haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.” Unabii wa
Agano la kale wamtaja Yesu kama Mungu, “Kwa
ajili yetu mtoto amezaliwa. Kwetu mtoto
tumepawa na ufalme utakuwa mabegani
mwake. Na ataitwa Mshauri wa ajabu, Mungu
mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa
amani.”
Kwa hivyo, kama C.S. Lewis alivyosema, kumtaja
yesu kama mwalimu mwema tu si sawa. Yesu
alikiri waziwazi kuwa yeye ni Mungu. Kama si
Mungu basi ni muongo na si nabii, mwalimu
mwema wala mcha mungu. Wanavyuoni wa sasa,
husema, “Yesu yule wa kihistoria” hakusema
mengi ya yale biblia inyomtaja nayo. Sisi ni
wakina nani hata tupinge neno la Mungu
kuhusu kile Yesu alisema ama kufanya?
Mwanachuoni huyo wa miaka zaidi ya elfu mbili
baada ya Yesu atakuwa na mtazamo gani wa
kweli kushinda wale walioishi na kumtumikia
Yesu kristo huku wakifundishwa pia (Yohana
14:26)?
Ni kwa nini, swali juu ya Yesu ni nani, ni
muhimu? Kuna tatizo gani kama Yesu kweli ni
Mungu au la? Swala muhimu linalompasa Yesu
kuwa Mungu ni kwamba, kama si Mungu, kufa
kwake hakungetosha kufidia dhambi za
ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2).
Mungu tu ndiye angeweza kufidia adhabu hiyo
(Warumi 5:8; Wakorintho wa pili 5:21).
Ilimlazimu Yesu kuwa Mungu ili alipe deni zetu.
Yesu ilimbidi awe mwanadamu ili afe. Wokovu
wapatikana tu kwa imani juu ya Yesu kristo!
Uungu wa Yesu ndio unao sababisha yeye kuwa
Njia ya pekee ya wokovu. Uungu wa Yesu ndio
uliomfanya kukiri, “Mimi ndimi njia kweli na
uzima. Hakuna ajaye kwa Baba ila kupitia
Mimi” (Yohana 14:6).

Post a Comment

0 Comments