Muimbaji mkongwe mzaliwa wa nchini Benin, Angelique Kidjo ameshinda tuzo ya tatu ya Grammy.
Ameshinda kipengele cha Best World Music Album kwa santuri yake ya ‘Sings’ ambayo imekusanya nyimbo zake zilizochanganya na mahadhi ya classic ya Ulaya na kushirikiana na bendi ya Orchestre Philharmonique du Luxembourg.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Kidjo kushinda kipengele hicho baada ya mwaka jana album yake ya ‘Eve’ iliyokuwa ikiwapa heshima wanawake wa Afrika kushinda.
“Thanks to my fans! I m dedicating my #Grammy to my fellow African artists and musicians! I love and respect you so much! You inspire me,” ameandika Kidjo kwenye Instagram.
Vanessa Mdee amempongeza muimbaji huyo kwa kuandika, “Queen on a MILLION Levels @angeliquekidjo God Bless You Mama [purple_heart] And Congratulations on another #Grammy you inspire us soooooo much. Asante Sana.”
Muimbaji huyo ameshatoa zaidi ya album 10 hadi sasa.
0 Comments