Jonas Malheiro Savimbi alikuwa ni kiongozi wa vita vya msituni nchiniAngola. Savimbi alizaliwa 3 Agosti 1934na kufariki 22 Februari 2002. Mwaka 1966alianzisha vuguvugu la UNITA (kireno: União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.
De Jonas Savimbi mnamo mwaka 2000
UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana. UNITA ilianza kama kikundi chenye itikadi ya kikomunisti kufuatana na itikadi ya Mao Zedong. Uadui kati ya wakomunisti wa Uchina na Urusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya MPLA iliyosaidiwa na Urusi. Baada ya uhuru mwaka 1975 MPLA ilitawala mji mkuu na serikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
Savimbi alipata a kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali duniani ili kuiondoa madarakani serikali ya MPLA(kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho).
Savimbi alikuwa akipata misaada ya fedha na silaha toka serikali za Marekani, China, Afrika Kusini, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikijulikana kama Zaire),Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba, na Nicaragua.
Savimbi aliuawa vitani 22 Februari 2002.
0 Comments