Muhammad Ali (amezaliwa na jina laCassius Marcellus Clay Jr.; mnamo 17 Januari 1942) ni mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. Amepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Huyu anatazamika kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote. Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano yaOlompiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini Rome, Italia. Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, amekwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la "Mwanamichezo wa Karne" na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.[1]
Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni "napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki".[2]
Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu yaNation of Islam mnamo mwaka wa 1964, baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975. Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uwanamasumbwi, na leseni yake ya uwanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.
0 Comments