Malkia Cleopatra ni maarufu zaidi kati ya malkia wote waliowahi kutawala Misri.
Cleopatra alizaliwa Alexandria mwaka wa 69 K.K (kabla ya kristo),Wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII. Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa . Cleopatra hakua Mmisri, ispokuwa mMacedonia familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander the Great.
Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.

Mfalme wa Misri ,Ptolemy wa XII ,anakufa mnamo mwaka wa 51 K.K. anaacha utawala kwa kijana wake mdogo mwenye miaka 12 Ptolemy XIII. Lakini anaagiza kwamba, kijana huyu atawale pamoja na dada yake mkubwa, Cleopatra. Pia ni lazima amuoe, kama desturi ya utawala wa ukoo wa Ptolemy, ingawa ndoa hiyo ilikua ni kama kuigiza.
ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.
ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.
Cleopatra mwenye miaka 18 mapema anathibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususani katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania. Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.
Caesar na Cleopatra: 48-44 K.K
Kuwasili kwa Julius Caesar Alexandria, kunampa fursa Cleopatra kuonekana Ulimwenguni ,kwa wakati huo. Anaachia Misri, mikononi mwa Julius Caesar ambaye baada ya kushinda vita Pompey anakua mtawala mwenye nguvu katika dola ya Roma.
Julius Caesar anaamua kupumzika kati ya 47 – 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyu hata kuangamiza majeshi ya kaka yake (ambaye hakuweza kufua dafu).
Julius Caesar anaamua kupumzika kati ya 47 – 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyu hata kuangamiza majeshi ya kaka yake (ambaye hakuweza kufua dafu).
Mara baada ya Caesar kuondoka Alexandria , Cleopatra anajifungua katika majira ya Kiangazi mnamo mwaka wa 47 K.K, anadai kuwa mtoto ni wa Caesar, na pia anamfanana sana .
Katika mwaka wa 46 K.K Caesar anamualika Cleopatra Roma pamoja na mwanae (ambae mara baada ya kuzaliwa alipachikwa jina Caesarion, “Caesar mdogo) ambao walikaribishwa katika jumba la kifahari likiwa na kila aina ya anasa. baadae caesar anauwawa.
Baada ya Caesar kuuwawa mwaka wa 44, Cleopatra aliamua kurudi Misri na mwanae.

ANTONIUS NA CLEOPATRA, 41- 31 K.K
Misri ya Cleopatra bado ni utawala ambao ni huru. Lakini karibu kila sehemu ya ukanda wa Mediterrania unajihusisha na siasa za Roma na kuna uvumi umeenea Roma kwamba Cleopatra amemsaidia “Cassius, mmoja kati ya waliomuua Caesar.
Katika majira ya kipupwe mnamo mwaka wa 41, Marcus Antonius anaamuru majeshi ya Roma kwenda upande wa Mashariki, na anaamuru Cleopatra aje aeleze juu ya tuhuma dhidi yake katika makao makuu yake huko Anatolia.
Cleopatra anavuka medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana simanzi.
Cleopatra anavuka medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana simanzi.
Kambi ya Antonius iko Tarsus, maili kadhaa kwenda mto Cydnus. Malkia anawasili akiwa katika Boti ya kifahari , akiwa amevaa mavazi yakuvutia ya mahaba , yenye asili ya Kigiriki. Hazuiliki kutamanika, na mapenzi yake mara yanaangukia ndani ya nyumba ya jenerali Marcus Antonius.
Cleopatra anamualika Antonius amtembelee Alexandria.
Anakubali mwaliko wake kwenda Misri kumtembelea, na anawasili Alexandria wakati muafaka kwa ajili ya kupumzika wakati wa majira ya Baridi.
Baada ya Antonius kuondoka kurudi Roma, Cleopatra patra anajifungua mapacha, mvulana na msichana. Wanakaa muda mrefu, hadi mwaka wa 37 K.K ndipo Cleopatra na wanawe wanaungana tena na Antonius.
Antonius Anamuagiza kuja Antioch, Syria ambako huko anamuoa.

Sasa wanajionesha waziwazi pamoja. na wanaungana kumpinga Octavian, mpinzani mkubwa wa Antonius katika Roma.
Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki , anakua na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa mashariki ya kati (Syria).
Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki , anakua na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa mashariki ya kati (Syria).
Katika desturi ya tawala nyingi za Mashariki, Cleopatra na Antonius sasa wanakua na uwezo wa kuabudu katika miungu mmoja. Katika Ugiriki wanakua “Dionysus (Antonius) na Aphrodite (Cleopatra), katika desturi za wamisri wanakua Osiris na Isis, hali kadhalika.
Makutano katika Alexandria 44 K.K
Makutano wengi wanakusanyika katika Alexandria, macho yao yakiangalia yanayojili toka kwa utawala huu, Katika jukwaa kuu ameketi Antonius na Mkewe Cleopatra akiwa amevaa mavazi ya sherehe maalum mithili ya miungu wa kike wa Misri.
Na katika viti vingine vinne vya kifalme wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na “Caesar –mdogo”, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.
Na katika viti vingine vinne vya kifalme wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na “Caesar –mdogo”, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.
Mnamo majira ya jioni katika tafrija hii, ambayo baadae ilijulikana kama “harambee katika Alexandria”, Antonius anaugawa utawala wa Medditerania Mashariki kwa familia yake hiyo mpya.
Antonius anamtangaza Cleopatra kuwa “Malkia wa Wafalme, na “Caesar-mdogo kuwa Mfalme wa Wafalme, kwa pamoja wakitawala Misri na Cyprus. na tawala zingine kwa watoto wao. Kwa Alexander, kijana wake mkubwa (umri miaka 6), anampa sehemu ya mashariki mwa Euphratia; kwa Mapacha, dada zake Alexander, Cleopatra, anawapa Libya na Tunisia, na kwa kijana wake mdogo, Ptolemy Philadelphus (miaka 2) ambaye amevaa mavazi ya kihistoria ya Macedonia, anamgawia Syria na sehemu kubwa ya Anatolia.

Inakua sherehe inayovutia, lakini ambayo baadae italeta uhasama na vita.
Actium na baadaye: 31-30 K.K
Mapigano kati ya majeshi ya Octavianus na yale ya Antonius na Cleopatra yanafanyika Actium, Ugiriki katika mwezi September. Pande zote mbili, wana majeshi makubwa ya miguu na yale ya farasi, lakini pia swala jingine ni meli za kivita za Roma, waliokuwa nazo pia.
Antonius na Cleopatra wanafaida ya kuwa na meli 500, 100 zaidi ya zile za Octavianus ambazo ni 400. Hizi ni zana za mbao ambazo ni imara sana. Zikiongozwa na na jeshi mahiri linalofikia askari hadi ya 250. Antonius anapanga jeshi lake la meli, pamoja na Cleopatra na majeshi yake nyuma, hazina kubwa ya Misri, tayari kwa mapigano.
Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki.
Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki.
Katika mapigano ya Actium meli za Octavianus zilishinda;
Katika hatua flani, Antonius anamjulisha Cleopatra juu ya meli zake , na mpango wakuvunja mapigano na kutoroka nae.
Antonius na Cleopatra wanafanikiwa kurudi, katika milki ya Cleopatra. Lakini wote wanaamua kujinyonga katika mwaka unaofuata, wakati Octavianus alipowasili Misri na jeshi lake. Marcus Antonius anaamua kujiua, malkia alijaribu kumshawishi kutofanya hivyo, lakini ilishindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuoneshwa kama mfungwa mbele ya halaiki. Hapa aliamua kufa tar. 12 Agosti 30 KK.
“asp” nyoka aliemuu Cleopatra 30 K.K
Cleopatra anaamua kujiua , kama ishara ya ushujaa mkubwa. Mara nyingi alichukulia “serious” uwajibikaji wake kwa Misri. Na pia ndiyo mtawala pekee wa kutoka ukoo wake aliejifunza na kujua kuongea lugha ya Misri.
Malikia anatambua kama akiwa hai tayari atakua mfungwa wa Octavianus.
Akilindwa na askari wake wachache katika sehemu ndogo ya makazi yake, anaagiza sumu ndogo ya nyoka, asp, ambayo inaingizwa kwa siri kupitia kwenye kikapu chake anachotumia kuletewa matunda.
Cleopatra anavaa mavazi yake mazuri ya ki-malikia, na analala katika kiti chake cha dhahabu. anamweka “asp” katika maziwa yake. Akijitoa kafara kwa “Amen-Re” mungu wa jua wa Misri.
Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (asp).
Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (asp).
Muda wa mwisho wa uhai wa Malkia unakua kama “maigizo”, na unakumbukwa sana katika historia ya maisha yake. Na pia unaweka kikomo cha utawala wa Ptolemy katika Misri.
Octavianus alimtafuta pia Caesarion kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake, akamuua. Akawachukua watoto wote watatu wa Marcus Antonius, akawaonesha mbele ya halaiki ya Roma kuonesha ushindi wake.
Pia anaichukua Misri kuwa sehemu ya utawala wa Roma, na kuchukua milki zote za ufalme wa Misri.
0 Comments