Mjue kiufupi VITALIS MAEMBE

VITALI MAEMBE Mswahili.
Alizaliwa Mwazye,Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa 20August 1976 nchini Tanganyika akasoma kidogo Chuo Cha Sanaa Bagamoyo.
Akitumia jina Vitali Maembe&The Spirit ametoa album 6 za Muziki katika mtindo wake aliouita Motokaa Muziki,Bagamoyo 2004-06,Imbila 2007,Kiporo mchanganyiko wa Imbila na Bagamoyo 2009,Chanjo 2010,Acoust motokaa2012,Vita 2013 katika mtindo ambao watu wameubadilisha jina kutoka Motokaa muziki na kujaribu kuita Chanjo Muziki.
Amekuwa akiimba muziki wa ridhaa kwa ajili ya Waafrika na nchi yake.
Anafundisha darasa la msingi wa Sanaa la watoto na vijana.Jua Art Foundation for Children.

Mwalimu,mchoraji,muigizaji,mwanamuziki,mwanasoka na mshairi.
Kwa sababu ya muziki wake amewahi kulamatwa na kushushwa jukwaani na Polisi mara mbili na kupelekwa kituoni kwa maelezo Kiteto,Manyara 2010 na Nzega,Tabora 2011.
Na amewahi kuzuiliwa mara kadhaa kufanya maonesho yake ya muziki.
Mwaka 2010-12 aliutumia kuzunguka nchini mwake Tanganyika kufanya maonesho ya muziki kupambana na rushwa.

Aliwahi kuondoka kwenye maonesho,miji,nchi mara kadhaa kujiepusha na hali ambayo ilikuwa ikitishia uhai wake,maisha yake ya sanaa na maisha yake ya mapambano.Hakuna kati ya wapenzi wake aliyekubaliana naye kuwa yupo hatarini.
2011 kutoka Tanzania alienda Sweden na Germany.
2012 kutoka Dar es Salaam na Bagamoyo alikikokuwa anaishi na kwenda Mahenge kisha Mbingu Morogoro.Aliandika shairi la "Jinamizi la Mwoga".February 2013 alikimbilia Kigali, Rwanda ambapo aligundua makazi bora na salama kwake.Kabla ya kurudi nyumbani kuendeleza mapambano dhidi ya falme za rushwa,wababe wapesa,imani dhalimu na mamlaka kandamizi.

Alienda Stockholm, Sweden kikazi na kuhofia kurudi nyumbani kwa wakati unaojulikaana baada ya kushikwa na "Jinamizi la woga" alikaa Norway na Ujerumani akiendelea kuandika 'Shajara' na kufundisha watoto na vijana ngoma na muziki wakati akifanya mpango wa kwenda Kigali Rwanda.
Kabla ya kurudi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndani yake ilipaswa iwe na nchi yake iliyofichika Tanganyika kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kama alivyopanga.

Aliporejea nyumbani na kuendelea na mapambano kwa sauti,kalamu na karatasi alianza kusakwa ilyopelekea kukikimbilia Ruangwa na baadae Farm 17 Nachingwea na kufanikiwa kujipenyeza kutimkia Norway huku akikosa haki yake ya kikatiba ya kupiga kura 2015 kuchagua viongozi wake.

Maembe Vitali
Mwenye Muziki Wake
Chanjo Ya Rushwa
Sumu ya Teja.
NAKUOMBE HERI NA BARAKA KTK HARAKATI ENDELEVU.
(Hakuna kuongopa,hakuna kuogopa)

Post a Comment

0 Comments