Mtoto wa Obama Arekodiwa Akivuta Bangi

Mtoto mkubwa wa Rais Barack Obama – Malia Obama – anahisiwa siku kadhaa nyuma alikuwa amepewa kipisi cha bangi kuvuta na akavuta na kujikuta akirekodiwa na video za mapaparazi wa Marekani. Tukio hilo limekuja siku chache tu baada ya video nyingine kumuonesha binti huyo akikata viuno kwenye moja ya matamasha ya muziki huko Marekani.

Inasadikiwa Malia alivuta sigara hiyo ‘haramu’ kwenye tamasha la lollapalooza kwenye Jiji la Chicago, jimbo la Illinois ambalo ni jimbo la nyumbani kwa Rais Obama. Mmoja wa wahudhuriaji wa tamasha hilo Jerrdin Selwyn mwenye umri wa miaka 18 alidai kuwa alimkuta Malia akiwa anavuta ganja na marafiki zake na hakukuwa na shaka ya hilo kwani harufu ya bangi ilikuwa wazi.

“Kulikuwa na kijana mmoja pale ambaye alikuwa anavuta na akampasia Malia ambaye alishikilia kama kwa dakika moja kisha akampatia mtu mwingine” alidai binti huyo. Na alidai pia kuwa alikuwa na picha zinazoonesha mtoto huyo wa Rais wa Marekani akivuta bangi hiyo.

Jimbo la Illinois lilipunguza adhabu ya na kuondoa kama kosa mtu akikutwa na chini ya gramu kumi za bangi na adhabu zikapunguzwa ambapo sasa faini ya kati ya dola 100 na 200 hutozwa kwa mtu ambaye anakutwa nayo kama matumizi yake binafsi. Majimbo kadhaa nchini Marekani yamejaribu kuondoa kukutwa au kutumia bangi kama kosa la kisheria na majimbo mengine yanaruhusu matumizi ya bangi kwa ajili ya kupunguza maumivu ya magonjwa mbalimbali na hivyo wanaruhusu bangi kwa matumizi ya kitabibu (medicinal purposes). Baadhi ya majimbo yenye sheria hiyo mpya ni pamoja na Michigan, California, na Colorado.

Hata hivyo, kwa baadhi ya watu habari hii inaweza isiwatushe sana kwani tayari Obama mwenyewe aliwahi kukiri kuwa alipokuwa kwenye shule za sekondari alikuwa na kundi la vijana wenzie ambao walikuwa wanakunywa na kuvuta bangi.

Malia amemaliza sekondari ya Juu mwaka huu na ameamua kuchukua mwaka nje ya chuo kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu ambacho alisoma baba yake na mamake cha Harvard mwakani kuendelea na masomo.

Siyo watu wote wanaonekana kukwaza na kitendo hicho kwani wengine wanaona ni tabia tu ya ujana na kuwa ataachana nayo huku watu wengine wanaona kama mtoto wa Rais anaonesha mfano mbaya kwani wapo watoto wengine wa walalahoi ambao wamekutwa na gharama kubwa kwa kukutwa wakivuta bangi.

Post a Comment

0 Comments