Wananchi wa kiponza (chamanzi,Dar es salaam) warudisha kadi za ccm
Kadi hizo zimerudishwa kwa mwenyekiti wa mtaa mpaka katika ngazi za wilaya (temeke)
Sababu kubwa ya wananchi kurudisha kadi hizo ni kutokana na kitendo cha Diwani wa kata ya chamanzi kuwaongelea maneno machafu wananchi kwa kuwaita kunguni
sababu ya diwani huyo kuwaita kunguni wananchi ni pale wananchi walipolalamika kwa kuondolewa stand ya mabasi madogo maeneo ya kiponza sokoni na kurudishwa maeneo ya Mbande mwisho
kurudishwa kwa soko na stand hiyo ilikuwa ni moja kati ya sera za diwani huyo kabla ya uchaguzi
lakini leo hii wananchi wameona kama wamegeukwa na kuamua kurudisha kadi hizo za ccm wakiongozwa na mwenyekiti wao
0 Comments