Yaliyojiri Kutoka Ufipa: Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari, maandamano ya UKUTA yaahirishwa

Amaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa CHADEMA
taifa na anaongelea uamuzi wa jeshi la wananchi
kufanya usafi na urushaji wa ndege siku ya leo
ambayo anasema haijawahi kufanya tangu uhuru.
Anasema anavyozungumza, katibu mkuu(Salum
Mwalimu) anaendelea kushikiliwa na polisi mji wa
Bariadi na ilikuwa leo apelekwe mahakamani lakini
polisi wamesema wako bize.
Freeman Mbowe amesema maandamano ya UKUTA
yameahirishwa kwa mwezi mmoja hadi tarehe
Oktoba Mosi.
Mbowe: Tumepata wakati mgumu kufikia uamuzi, sio
kila wakati viongozi tutafanya mambo
yatayowapendeza wanachama wetu. Viongozi wa dini
awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa
UKAWA warejee bungeni. Kamati kuu ya CHADEMA
imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini.
Mbowe: Ni matumaini yangu wana CHADEMA
watatuelewa kamati kuu, asanteni sana kwa
kunisikiliza.
Kinachoendelea kwa sasa ni maswali kutoka kwa
waandishi wa habari.
Kwa nini hamjapeleka shauri mahakamani: Mbowe:
Yamepelekwa mashauri mengi mahakamani na
yataendelea kupelekwa. Hatuwezi kuwalazimisha
mahakama, hata kipindi hiki kuna mashinikizo kwa
baadhi ya mahakama watoe maamuzi watoe maamuzi
yanayorandana na serikali, wapo waliosimamia sheria
lakini mahakimu nao ni binadamu.
Mimi ni miongoni mwa watu ambao tulitamani kesho
watu wawe barabarani, wanachama wetu ambao
watakwazika, UKUTA sio CHADEMA, UKUTA ni
mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya
watanzania. Sasa hayo makundi yamekuja
kutushauri tuwe pamoja, sisi ni nani tukatae. Watu
kama Mwl Nyerere foundation wametusihi, hata
Lowassa amaengea na mama Maria Nyerere
wametusihi.
Mbowe: Viongozi waliomba wiki mbili mpaka tatu
lakini sisi tukasema hapana kuna wengine tutakuwa
na majukumu bungeni na hili jambo ni la kitaifa.
Hatuna nia ya kuchafua Taifa, tuna nia ya kusaidia
Taifa.
Mbowe: Mpaka jana tulikuwa na viongozi 230 amabao
wameshtakiwa, viongozi 28 mapaka jana walikuwa
hawajaachiwa kwa mujibu wa takwimu zetu akiwemo
naibu katibu mkuu Zanzibar.
Mbowe: Nisikitike siku za karibu mahasimu wetu
wamekuwa wakijaribu kutugombanisha ndani ya
CHADEMA, hizi fitna za mitandao. Mbowe sina tabia
ya kutoa matakamko nje ya taratibu za chama,
Tamko nililotoa ni la leo.
Lowassa: Mitandao inaandika mambo mengi sana
ambayo ni just accusations, ningekua na muda
ningefafanua.

Post a Comment

0 Comments