Mkenya anayefahamika kwa jina la Alexander Kinyua (22) amekiri kumuua na kula moyo na ubongo wa Kujoe Bunsofe Kodie (37) mzaliwa wa Ghana huko marekani katika nyumba ambayo walikuwa wakiishi pamoja
Kinyua alikiri kuhusika na mauaji katika. Jimbo la Maryland mwaka jana aliposhtakiwa lakini jaji akasema hafai kulaumiwa aliposhtakiwa jumatatu ya wiki hii.
Jaji Stephen Waldron alisema Kinyua hafai kulaumiwa kwa sababu ana matatizo ya akili na akaagiza apelekwe kwenye hospitali ya watu wenye matatizo ya akili.
Kinyua alikuwa anasomea uhandisi katika chuo cha Morgan State alisema alitumia kisu kumuua mwenzake na kisha akala viungo vyake
Awali Kinyua alikataa kuhusika na mauaji lakin baadaye alikiri na kuwapeleka maafisa katika jaa la kanisa ambalo alificha mwili wa marehemu
Uchunguzi wa hali ya kiakili ulibaini kuwa Kinyua alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa uitwao "Paranoid Schizophrenia"
0 Comments