Mjue Dedan Kimathi: aliyekawa kiongozi wa mau mau

Dedan Kimathi (31 Oktoba 1920 – 18 Februari 1957) alikua Mkenya aliyeongoza harakati za kundi la Mau Mau za kutwaa ardhi iliyokuwa iko mikononi mwa wakolonitoka Uingereza. Kimathi alihukumiwa na kunyongwa kutokana na harakati zake za kuikomboa nchi ya Kenya. Waingereza, Serekali ya wakoloni ilimchukua Kimathi kama mgaidi, lakini wananchi wengi wa kabila la Gikuyu walimchukua Kimathi kama mpigania uhuru. Alizaliwa mnamo 31 Oktoba 1920 katika kijiji cha Thenge huko tarafa ya Tetu, wilaya ya Nyeri na alinyongwa na Waingereza tarehe 18 Februari 1957.

Maisha ya mwanzo

Alipofika miaka kumi na mitano, Kimathi alijiunga na shule ya msingi, Karuna-ini, ambapo aliweza kustadi kiingereza halisi. Hii baadaye ilimsaidia kuandika kwa kiingereza kabla ya mnyanyuko na wakati wa mnyanyuko wa Mau mau. Akiwa shuleni alijiunga kwa chama cha ushauri. Alikua muumini wa dini na alibeba Bibilia kila wakati. Alifanyia kazi idara ya misitu kuokota begu za miti, ili aweze kujilipia gharama ya shule. Baadaye akajiunga na shule ya upili ya Tumutumu CSM, lakini akaacha shule kwa sababu ya kutolipa gharama ya shule.

Kimathi alifanya kazi kadhaa lakini hakupata msimamo. Mojawapo ya kazi hizo alijiunga na jeshi na kutumwa kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka wa 1941. Lakini, mwaka wa 1944, alifukuzwa jeshi kwa sababu ya makosa kadhaa. Mnamo1946, alijiandikisha kwa chama chaMuungano wa Waafrika Wakenya. Mnamo1949, alianza kufunza shule alikosomea, lakini wakamfukuza kazi kwa sababu ya kulaumiwa amefanya ubakaji.

Maisha

Kimathi aliweza kuvutia watu kwa kuonyesha bidii kwa kazi aina zote, alizoweza kufanya. Kimathi alianza siasa za upinduzi mwaka wa 1950. Alianza kuwa mfuasi wa Mau Mau, na baadaye kupanda cheo na kueza kuwapa wajiunga wapyakiapo cha Mau Mau na kwa hivyo akawaharamia kulingana na Waingereza. Alijiunga tena na Kikundi ya Arubaini, wakombozi wa Chama cha Kati cha Wakikuyu mwaka wa 1951. Alichaguliwa kama karani kwa chama cha KAU eneo ya Ol' Kalou na eneo ya Thomson Falls mwaka wa 1952. Alishikwa kwa mmda mwaka huo, lakini akatoroka kwa usaidizi wa polisi wa kijiji. Hii ilileta mwanzo wa Vita vya ukereketwa halisi. Kimathi aliunda baraza yaulinzi wa Kenya, ambayo ilitoa amri kwa wapiganaji wate msituni, mwaka wa 1953.

Mwaka wa 1956, alishikwa pamoja na bibi yake mmoja, Wambui. (hadithi nyingi za Kimathi za eleza vile alivyopigwa risasi.) Alihukumiwa kifo na mahakama, na Jaji wa sheria Chifu Kenneth O'Connor, akiwa bado kitandani katika hospitali kuu yaNyeri. Asubuhi na mapema mnamo 18 Februari 1957 Alinyogwa na Serikali ya wakoloni Waingereza.

Urithi

Kimathi alizikwa kwenye kaburi la umma mahali pasipojulikana katika gereza la Kamiti. Serikali ya Uingereza mpaka sasa inapinga maiti ya Kimathi ifukuliwe ili azikwe tena kirasmi, kwasababu wanasema alikuwa gaidi. Lakini Wakenya wengi wamchukulia kuwa Shujaa wa Taifa. Jina la Kimathi linakumbukwa nchini Kenya hasa kutokana na Mitaa ya Miji, majengo mengi na pia barabara ambazo zimeitwa kwa jina lake. Mchezo wa Kuigiza wa "Mzalendo Kimathi" ama kwa kiingereza The Trial of Dedan Kimathi umeandikwa na Ngugi wa Thiong'o (ndugu wa shujaa wa Mau Mau) akishirikiana na Micere Mugo na mchezo huo unaeleza kisa cha Kimathi

Post a Comment

0 Comments