“Mtu asiyesimamia chochote basi ataanguka kwa chochote.”
□ □ □
“Hakuna atakayekupa uhuru, hakuna atakayekupa usawa na haki, kama wewe ni mwanaume nenda uichukue.”
□ □ □
“Sababu za wazayuni kuhalalisha uvamizi wa Izrael katika ardhi ya Palestina hazina mashiko ya kiakili wala kihistoria.”
□ □ □
“Hautakiwi uwe kipofu kwa uzalendo wa nchi yako mpaka unashindwa kupigania ukweli. Baya ni baya tu, haijalishi liwe liwemafanywa na nani au kusemwa na nani.”
□ □ □
“Shule yangu ilikuwa vitabu na maktaba nzuri…nilitumia maisha yangu yote kule nikiwa nasoma, nikitimiza azma yangu ya udadisi.”
□ □ □
“Elimu ni pasipoti yetu ya baadae, kwani kesho iko kwa ajili ya wanaojitayarisha nayo leo.”
□ □ □
“Tangu nikiwa mdogo nilijifunza kama unahitaji jambo basi fanya kelele.”
□ □ □
“hatuwi na fujo kwa mtu ambaye hatufanyii fujo.”
□ □ □
“Dhumuni letu ni kuwa na uhuru kamili, usawa na haki kwa njia yoyote ile itakayohitajika.”
□ □ □
“Ukweli upo katika upande unaoonewa”
□ □ □
“Huwezi kutenganisha amani na uhuru wa kweli, kwa maana hakuna atakayekuwa na amani kama hana uhuru.”
□ □ □
“Hutakiwi kuwa mtu tu, eti ili upiganie haki yako, unachotakiwa kufanya ni kuwa mtu mwerevu, mjanja.”
□ □ □
“Kama hautakuwa tayari kufa kwa ajili yake, basi liondoe neno ‘uhuru’ katika kamusi yako”
□ □ □
“Gharama ya uhuru ni kifo.”
□ □ □
“Mimi ni yule mtu niliye kama wewe
unavyofikiri ulivyo…Ukitaka kujua nitakufanya nini, jaribu kufikiria
ingekuwa wewe ungefanya nini. Nitafanya hilo hilo kwako tena nitaongeza
kidogo.”
□ □ □
“Hata iwe heshima ya ukubwa gani
wanayoionesha kwangu mimi, hata uwe utambuzi gani wanaotumia hawa
wazungu kutambua uwepo wangu mimi, ili mradi bado heshima hiyo
haioneshwi kwa kila mmoja wetu bado siooni na siihitaji heshima hiyo
kwangu.”
□ □ □
“Haimaanishi kuwa nahamasisha utumizi
wa nguvu na vurugu, lakini pia sipingi kutumia njia hii kwa ajili ya
kujilinda. Siiti njia hii ni ya vurugu tunapoongelea kisasi bali naiita
ukuaji wa akili.”
□ □ □
“Utamshukuru vipi mtu kwa kukupa kitu
ambacho tayari chako? Na cha kushangaza ni pale unapawaona watu
wakishukuru kupewa sehemu tu ya kile ambacho tayari ni chao.”
□ □ □
“Ni muda wa kufa shahidi sasa, na kama
ikatokea kuwa miongoni mwao, basi itakuwa kwa ajili ya udugu wetu. Na
hilo ndilo jambo pekee litakaloweza kuokoa taifa hili.’
□ □ □
“Haiwezekani ubepari uendelee kuwepo,
kimsingi huu mfumo wa ubepari unahitaji damu ya kunywa. Ubepari ulikuwa
kama tai, lakini sasa umeshakuwa kinda lake. Ulikuwa na nguvu ya
kunyonya damu ya yeyote bila kujali unanguvu au la. Lakini sasa umekuwa
mfumo wakioga, ukinyonya damu ya wasiojiweza tu. Kwa uhuru
huu,unaowafikia mataifa mbalimbali, ubepari umekuwa ukijeruhi wachache,
unanyonya damu ya wachache, na unakuwa dhaifu kila siku. Naimani kwa
kipindi kifupi, utamalizika kabisa.”
□ □ □
“Mfumo
mpya wa maisha uko njiani kuja, ni jukumu letu kujitayarisha ili
tuchukue sehemu zetu, tulizo na haki nazo katika maisha hayo.”
□ □ □
“Mimi ni mfuasi wa ukweli, bila kujali nani kausema.
Natetea haki, bila kujali nani anapinga au nani anatetea. Mimi ni
mwanadamu, na naunga mkono yeyote au chochote kitakacho mfaidisha
mwanadamu.”
□ □ □
“Naamini dini inayoamini uhuru. Kwa
dini yoyote ambayo haitaniruhusu nipigane kwa ajili ya kutetea watu
wangu, bora na iende tu dini hiyo.”
□ □ □
“Mimi ni Muislamu, kwa sababu ndiyo
dini inayofundisha jicho kwa jicho na jino kwa jino. Inakufundisha
kuheshimu kila mtu, na kujali haki za wote. Lakini pia inafundisha iwapo
mtu akitokea akakukanyaga kwa kukuonea, kata miguu yake. Nitabeba shoka
la dini yangu kila mahali.”
□ □ □
“Hakuna mafundisho katika kitabu chetu yanayotuagiza tuumie kimya kimya. Dini yetu inatufundishe tuwe waerevu.
Kuwa mtu wa amani, kuwa na huruma, tii sheria, na umuheshimu kila mtu;
lakini akitokea mtu na kunyanyua mkono wake kwako usisite kumpeleka
kaburini.”
□ □ □
“Mimi ni Muislamu na nitaendelea kuwa hivyo. Dini yangu ni Uislamu.”
□ □ □
“Sio tu Marekani ndio wanaotakiwa kuufahamu na kuuelewa Uislamu bali ni watu wa dunia nzima.”
□ □ □
“Kwa kila umuonapo mtu anafanikiwa kuliko wewe, huwa anafanya jambo ambalo wewe hulifanyi.”
□ □ □
“Kukaa tu mezani hakukupi chakula.
Unatakiwa ukile kile kilichokuwa katika sahani. Kuwa hapa Marekani
hakukufanyi wewe uwe mmarekani. Kuzaliwa hapa marekani hakukufanyi pia
uwe mmarekani.”
□ □ □
“Kama nikifa huku nikifanikisha kuileta
nuru yoyote, nikiwa nimesambaza ukweli wowote utakaosaidia kuua sumu ya
saratani hii ya ubaguzi inayoshambulia mwili wa Marekani, basi shukrani
zote zinamstahiki Allah na makosa yote yatabaki kuwa yangu.”
□ □ □
“…Kwa njia yoyote ile itakayohitajika”
□ □ □
“Sifa zote njema zinamstahiki Allah, Mola wa walimwengu wote.”
□ □ □
0 Comments