Sio kila msanii anayerap anakuwa anawakilisha hip hop – Nash MC

Mwana hip hop nchini Nash MC aka Maalim Nash amefunguka kwa kusema kuwa sio kila msanii anayerap anauwakilisha muziki wa hip hop.

Rapa huyo amesema msanii wa hip hop hapimwi kwa kurap pekee bali kuna vitu vingine kama mashairi vinapaswa kuangaliwa.
“Kabla hujatoa mawazo yako lazima ujue unachokwenda kuzungumzia, ukizungumzia hip hop unalenga maisha ya watu” Nash alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM”. Huwezi kutokea zako ulipotoka ukatoa cheo cha hip hop kwa mtu ambae hafanyi hip hop. Sio kila msanii anayerap atakuwa anawakilisha hip hop, hip hop inawakilishwa na MC ambae kiswahili chake ni mchenguaji,”
Aliongeza, “Mimi leo hii siwezi kukurupuka nikasema Alikiba hawezi kuimba kwa sababu sipo katika upande wa waimbaji, huwezi kukurupuka tu ukatoa maoni, umetoa maoni wapi? Marehemu Banza Stone alikuwa anarap hata Khalid Chokoraa ila haiwezekani kila anaerap ukamuingiza kwenye hip hop,”
Rapa huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Hasi 15’.

Post a Comment

0 Comments