Wamakua Walikuwa Watundu au Walipelekwa Utumwa?

Utundu unazaliwa nao na wala huwezi kusomea au kujifunza utundu darasani, na hata kama utajitahidi kuiga au kujifunza utundu itakuwa si rahisi kuumudu na kuumiliki utundu siku zote! Utundu umeweza kuwafanya watu kuhangaika huku na kule kila kona ya dunia wakitafuta riziki na hata wakati mwingi si kutafuta tu riziki bali kutaka kujua au kuona ni jinsi gani watu au jamii zingine zinavyoishi nje ya eneo au maeneo husika.


Wamakuwa ni kabila ambalo lipo mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara, Lindi na Ruvuma, lakini pia kabila hili lipo nchi ya jirani ya Msumbiji,hili ni jambo la kawaida kwa makabila yote yaliyopo maeneo ya mipakani kwa vile wakati wakoloni wanagawa mipaka hawakuzingatia makabila, bali walizingatia urahisi wa mpaka kuonekana wakitumia vitu kama vile mito, milima, mabonde, maziwa, misitu, majangwa nakadhalika! Hivyo kulingana sababu hizo zimeweza kulitenganisha kabila moja kuishi katika nchi mbili; au kutokana na sababu hizo zimeufanya ukoo mmoja uishi katika nchi mbili tofauti; au kulingana na sababu hizo hizo zimewafanya ndugu wa damu kuishi nchi mbili tofauti na hata kushindwa kutembeleana wakati mwingine kulingana na taratibu za visa na mengineyo!


Kinachonishangaza zaidi ni kwamba nikivuka bahari ya Hindi na kuvikuta visiwa vingi ambavyo vimezungukwa na bahari hii ya Hindi kama vile kisiwa cha Komoro, kwenye kisiwa hiki lugha ya taifa ni Kifaransa, na lugha ya pili ni Kimakuwa ingawa pia kuna baadhi ya sehemu ambazo Kiswahili kinazungumzwa licha ya kwamba hakikunyooka na wakati mwingine waweza fikiri kwamba siyo Kiswahili!


Nikishuka chini upande wa kusini mwa kisiwa hiki ndani bahari hii ya Hindi nakikuta kisiwa kikubwa sana cha Madagascar, lugha ya taifa ya kisiwa hiki ni Kifaransa na baada ya hapo kuna lugha nyingi ndogo ndogo zinazozungumzwa nchini humo, inategemea ni upande gani wa nchi; ukiwa kaskazini mwa nchi hii pia kuna watu wengi tu wanaoongea Kimakuwa na wengine wanaongea pia Kiswahili kibovu lakini kinaeleweka!



Nikienda pia upande wa mashariki mwa kisiwa hiki cha Madagascar kuna kisiwa kingine cha Mauritius ambacho lugha ya kisiwa hiki ni Kifaransa kama lugha ya taifa, lakini pia kuna baadhi ya wenyeji wanaoongea Kimakuwa!



Nikiendelea kusini mashariki mwa kisiwa hiki cha Mauritius nakikuta kisiwa cha Reunion ambacho ni kisiwa cha Ufaransa na kipo katika jumuiya ya nchi za ulaya (EU) lugha ya taifa ya kisiwa hiki ni Kifaransa na wenyenji wengi wa kisiwa hiki ni watu weusi waliochanganyika na watu wa Asia na Ulaya; pamoja na hayo lakini baadhi ya watu wa nchi hiyo kuna wanaoongea Kimakuwa!


Sasa ndiyo maana najiuliza Wamakuwa walikuwa watundu sana au walipelekwa utumwa, na utumwa ulipopigwa marufuku wakabakia huko huko au ilikuwaje? Kama ambavyo raia wa Mali (Mandingos) walivyokuwa watundu na kuwa watu wa kwanza kugundua Amerika na pia kusafiri kwenda hadi India hata kabla ya Christopher Columbus na Vasco da Gama kufanya hivyo! Pamoja na kwamba Mandingos walikuwa watu wa kwanza duniani kustaarabika lakini ukweli huu umefichwa na badala yake kuhamishiwa Egypt! Sasa sijui kisa na sababu ya kuwanyongea Mandingos ni kwa vile ni weusi sana au ni kwanini!? Waispania na Wareno walipofika Mexico na Brazil wanakiri kwamba pamoja na kwamba waliwakuta wenyeji Wahindi wekundu, lakini walikuta sanamu na picha za watu weusi zimechorwa sehemu mbalimbali na kuhifadhiwa, lakini hapo hapo wanadai Christopher Columbus ndiye aliyegundua Amerika, licha ya kwamba Mandingos kutoka Mali walifanya biashara na Wahindi wekundu miaka 400 kabla ya Christopher Columbus kufika Amerika! Ina maana historia ya dunia pia imechakachuliwa!

Post a Comment

0 Comments