Mjue Nimrod



 

Huyu ni mpagani wa kale sana anaitwa Nimrod. Wanatheolojia na wanahistoria wengi wa wanamhusisha moja kwa moja na ujenzi wa mnara wa babeli. Babilon ndio kitovu cha upagani ulimwenguni, mji huu upo Iraq(ya sasa) maili 90 kusini mwa mji wa Baghdad.

Nimrod alijenga hii Babiloni, akajenga na Ninawi, akaenda Siria akajenga mji wa Ashuri na aliijenga pia Kaanani.
Nimrod ametajwa mara 4 ndani ya biblia,mara tatu ametajwa moja kwa moja. katika Mwanzo 10:8-12 na ametajwa pia katika Mika 5:6 na Nyakati 1:10, katika Qur'an ametajwa katika sherehe ya tafsiri ya aya ya 258 ya sura ya pili(baqarah) kama"Namrudha".
Huyu aliabudiwa kama mungu, kutokana na ushujaa wake wa uwindaji, na watu wa zama hizo walimfuata kama msaada badala ya Mungu, aliwalinda dhidi ya wanyama wakali.
Kwa mujibu wa wanahistoria alimuoa mwanamke aitwae Semiramis, inasemekana alikuwa ni mke wa baba yake aitwae Kushi, mtu mweusi wa zama hizo, zamani kwao ilikuwa kawaida mtu kumrithi mke baba yake yaani kumuoa mama yake mzazi.
Nimrodi alijiita mungu na aliabudiwa,alitaka kushindana na Mungu kwa kujenga mnara wa babeli,inasemekana aliona katika mbingu kipande cha nguo nyeusi na taji, akaamuru atengenezewe taji kama hilo na akawa mfalme wa kwanza ulimwenguni kuvaa taji, wasiojua kuhusu hilo walidai ameshushiwa toka mbinguni.
Nimrodi ana historia nyingi sana kwani aliishi miaka mingi lakini habari zake nyingi zilipindishwa na kutiwa chumvi na kukosewa kadiri muda ulivyosogea kuja karne zetu! alikuwa mkuu wa uwindaji na hodari "mighty hunter" na amekuwa wa kwanza akiitwa "mighty" tangu mafuriko ya Nuhu kutokea.
Biblia haitaji kuhusu mama yake(semiramis) au tarehe ya kuzaliwa Nimrod lakini masalia ya kumbukumbu za Wamisri na wababeli vinamtaja semiramis kuwa mama yake na Nimrod kuzaliwa december 25 inayosheherekewa Christmass leo!
Biblia wala Qur'an havitaji kifo cha Nimrod, lakini vitabu vya kale zaidi ya hivyo vinasema alikufa kifo kibaya sana,wengine wanasema aliuawa na mnyama mwitu na wengine wakadai Shemu alimwua kwa sababu aliwapelekea watu kuabudu ibada ya Baal.
Mama-mke (Semiramis) alimfanya mwanae au mumewe kuwa mungu baada ya kifo chake, na yeye alijipa uungu mke(goddess). alizaa mtoto kwa zinaa na kumuita Tamuzi akawa mwindaji hodari na pia mungu wa mavuno.Tamuzi alioa mke aitwae Ishtar kwa kigiriki Jupiter.
Nimrod akawa mungu baba, Semilamis mungu mama, na Tamuzi mungu mwana na mungu wa mavuno. nadharia ya imani hizi za kipagani zilianzia hapo.
Wanahistoria wanasema tamuzi alikuwa kipenzi cha wanawake sana(ezekieli 8:14),kifo cha Tamuzi kilitokea mawindoni, japo kuna utata kuhusu hilo! wengi wanadai aliuawa na nguruwe hivyo mama yake aliamuru wafuasi wale nguruwe sana kama sehemu ya kisasi...........

Post a Comment

0 Comments