Fahamu : Application anayotumia Trump

Kwa mujibu wa mwanahabari za kisiasa AXIOS Media, Mike Allen ameeleza kuwa application moja tu ndio inayotumika na kupatikana katika simu ya Rais wa Marekani, Dolnad Trump.

Rais Trump ni mtumiaji wa simu aina ya iPhone, na kwenye simu hiyo kuna application ya Twitter ambayo imeweka moja kwa moja kwenye simu. Muda mwingi tumeshuhudia rais huyo ambaye anapigwa na baadhi ya wananchi wake akitumia mtandao huo  kutweet.
Awali Trump alikuwa mtumiaji wa Samsung, mpaka anaapishwa alikuwa anatumia Smsung Galaxy S3 iliyotoka 2012. Baadae Rais wa taifa hilo kubwa alibadirisha na kuhamia kwenye  iOS.

Trump ameonekana akitumia muda mwingi kuangalia TV na sio kuchat kama ilivyo watu wengi, huwenda hii ndio sababu Rais huyo kafanikiwa zaidi katika biashara zake kutokana na kukosa muda wa kuingia katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Snapchat na mingine.


Post a Comment

0 Comments