Ni mpenzi wa sanaa au watu mashuhuri waliowahi kuishi na kufanya mambo makubwa hapo zamani? kama ndivyo jina la Leonardo Da Vinci na Michelangelo si mageni kwako
Sikumoja Leonardo alikuwa na Rafiki yake Giovana di Gavina. Walikuwa wanapita maeneo Fulani ya bank ya Spain karibu na kanisa la Trinita, watu mashuhuri kadhaa walikuwa wamekusanyika huku wakijadili mambo Fulani Fulani kama ilivyo kawaida ya wazee wa kazi (wanafalsafa na watu makini). Ubishi ukanoga wakamwita Leonardo awatatulie mambo kadhaa waliyojadili.
Wakati huo huo Michelangelo alikuwa anapita, Leonardo alisema: "Michelangelo ataweza kutuambia maana yake em tumuachie nafasi." Michelangelo, alidhani wamesema hivyo ili wamuingize mtegoni,
alijibu:
"Hapana, eleza mwenyewe (huku akimlenga Leonardo), Mzee wa sanamu na kazi zisizoisha, unajiona kama nani sijui. Umeunda sanamu na haujaimaliza na ndomana umeacha hiyo kazi kwa aibu kubwa. Na kuamua kuwapa kisogo na kuondoka. Leonardo alikaa kimya na kutabasam baada ya kuambiwa maneno hayo " (alinukuliwa katika The Notebooks of Leonardo da Vinci, Oxford University Press, 1952, trans. Irma A. Richter, p. 356) Tuendelee na utajua mkasa wa sanamu lisiloisha ulikuwaje.
Hii ilimfanya Michelangelo kuonekana mwenye wivu. Kwamaana alionekana mwenye hasira kwa Leonardo. Hasira zisizokuwa na sababu, msanii langa alisema ‘CHUKI KAMA SIGARA, NEVER DID NEVER WILL’ Lakini hadithi hii haisemi kwanini Leonardo alimwuliza Michelangelo aelezee maandishi yale na alimuuliza kwa tone ipi . Labda ilikuwa ya kuchochea kitu fulani, labda ilionekana kama kejeli. Inawezekana labda Leonardo hakumpenda Michelangelo lakini chuki ya Michelangelo kwa Leonardo ilionekana Dhahiri na aliitoa bila kificho kwa siku hiyo mbele ya umma wa mtume Mohamad.
Kwanini tunasema ni wivu, kwasababu Michelangelo alizaliwa na kumkuta Leonardo akiwa na shughuli zake, maarufu na anayesifiwa na kila mtu. Da vinci alikuwa mtangazaji, mwanasayansi, mchoraji na mambo mengine mengi yanayosababisha hadi leo hii kuwa mtu namba moja mwenye vipaji vingi na aliyeweza kuvisimamia vipawa vyake kwenye kila kazi aliyofanya.
Kazi za Langelo zote ni kama marudio tu kwa Leonardo kwa lugha rahisi tunaweza kusema hata alimuinspire. Leonardo alikuwa ameshafanya kazi nyingi sana, wakati Michelangelo alikuwa na kazi ya Sistine iliyochorwa juu ya jengo huko Vatican
alhamdulilah hii kazi inahistoria ndefu na haikuwa ya mchezo, Sanamu ya David mfalme Daudi baada ya kucheza na kubaki bila nguo, sanamu ya Musa na Pietà sanamu ya huruma inayomwonyesha Yesu akiwa amemlalia Mariam baada ya kusulubiwa msalabani… ni kazi nzuri lakini zinaweza kulipwa na kazi mbili tu za Leonardo (MONALISA au LAST SUPER).
Picha ya MonaLisa sio kubwa, ni saizi ya kioo kidogo cha chumbani . Leonardo alifanya kazi ya kuichora kwa miaka minne na bado hakuimaliza, japo ukiitazama utasema imeisha.
Ah, lakini saizi ya kazi ya sanaa haipaswi kujaliwa sana, kwasababu wanasema: picha nyingi kubwa ni ndogo kiumbo.
Karamu ya Mwisho (LAST SUPPER) ni kubwa-460 × 880 cm. Leonardo alitumia miaka sita kuichora kabla ya kukata tamaa kwa sababu hakuweza kupata kichwa sahihi cha Kristo (Tutamzungumzia Casare Borgia siku moja kama walivyomzungumzia na Machiaveli kwenye THE PRINCE). Alichora mchoro baada ya mchoro na alitumia siku nzima kutazama ukutani. Lakini karamu ya mwisho (LAST SUPPER) ni picha bora hadi leo hii.
Sistine Chapel yake ilipaswa kuwa Jiwe Kuu la Wapanda farasi kwa Duke wa Milan. Leonardo Alipatiwa kazi ya kutengeneza sanamu kubwa ya farasi kama aliyopatiwa Michelangelo, alitumia muda mrefu kuweka mambo sawa lakini bahati mbaya vifaa vya chuma kwaajili ya kumuunda farasi huyo vilichukuliwa na duke wa Milan kwaajili ya kutengeneza silaha za vita. ili wapambane na wafaransa.
Mfano wa udongo wa farasi huyo aliyeandaliwa na Leonardo ulisimama kwa miaka hadi ulipoharibiwa na wafaransa baada ya kuiteka ardhi ile. Alishindwa kuisimamia tena ile project na kufariki, bahati nzuri michoro yake ilitunzwa na miaka ya 90 (miaka 500 baadae) kuna mtaalam alifanikiwa kuisimamia project hiyo hadi kwisha. Huyo ndiye farasi Michelangelo alikuwa akizungumzia baada ya kuambiwa na Leonardo awasaidie kufafanua kitu (hadithi ya Codice Magliabecchiano).
0 Comments