Hatimaye Mahasimu wa Muda Mrefu Jay Z na Nas wamekutana tena kwenye Album ya Dj Khaled


 

Wimbo unaitwa SORRY NOT SORRY. Mpaka sasa nimeskiliza kipande cha Nas tu, navuta pumzi nimsikilize Jay. Licha ya bifu lao au mgongano kuisha toka miaka ya 2006 lakini hadi leo hii, wapenzi wa utamaduni na muziki wa Hip Hop hawaishi kuongelea msuguano huu uliotokea kwenye Album ya Nas (stillmatic) mwaka 2001 kwa kibao chake cha ETHER- naweza kusema ESTHER ni kati ya Diss Track 3 bora kuwahi kutokea duniani.


Nas alimchana baada ya Jay kumshambulia Nas vibaya sana kwenye wimbo wake wa TAKEOVER alioutoa mwaka huo huo 2001 kwenye album yake ya THE BLUEPRINT akimsema Nas kwa flow mbaya na kudanganya kwenye nyimbo zake kuwa anayoyaimba hajayaishi-ameyaona kupitia vitabu na vyanzo vingine. 


Jay pia alikuwa akijipima ubora na wasanii wote wa kizazi cha 90's kama Mobdeep- ndomana Nas kwenye Esther anamwambia Jay- inamaana wewe unataka kujifananisha na Biggie, Gayz, Cock-A-Fella Records na maneno mengi machafu na hii kuifanya Esther kuwa Wimbo mkali wa miaka yote


wenye kudiss Walisample watu kibao na kuifanya nyimbo ya kuwachana wengine Beat hili aliwahi kulitumia Eminem kumchana Jumanne Dupri (Jermaine) na hata hapa karibuni aliwahi kulitumia Remmy Ma kumdiss Nick Minaj na yeye aliita Shether.

Licha ya bifu hii kuwanufaisha wote wawili Jay Z alimwomba msamaha Nas na familia yake baada ya bifu kufika mbali na kujibizana maneno machafu kwenye nyimbo zao, mfano kwenye U Don't Know"Jay alisema (nimelala na mama yako Nas ukiwa mdogo)

Mwaka 2006 Nas alimshirikisha Jay kwenye wimbo wake wa Black Republican ulioachiwa kwenye album ya Hip hop is Dead. Mwaka 2007 Jay z naye akatoa album yake ya American Gangster na kumshirikisha Nas kwenye kibao cha I Do It For Hip Hop Wakaendelea kupeana shavu.

Japo watu hawajaacha kulizungumzia bifu la Ether, na wamekuwa wakilinganishwa muda wote licha ya wao kuyamaliza. Na sasa tunamwona Dj Khaled akiwakaribisha wawili hao kwenye Album yake ya KHALED KHALED.

Post a Comment

0 Comments