Alama za Nyota na Tabia za Watu:Tambua Misingi ya Tabia Zako

Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.

Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.

Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.

Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu. Hii si haba,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa.

[Soma pia:Madhara ya Mwezi Katika Hisia na Tabia za Binadamu:Kuna Ukweli? ,  Nyota na Kazi Zenye Mafanikio ]

Tabia Za Watu Na Alama Za Nyota

Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.

Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.

Alama hizi ni kama ifuatavyo:

Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Juni 20Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22Mashuke(Virgo):Agosti 23 – Sept 22Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21Mbuzi(Capricorn):Des 22 – Jan 19Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18

Makundi Ya Alama Za Nyota:

Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama:

Moto:Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisiMaji:Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndaniHewa:Imara na yenye kukuza au kuendelezaUdongo:Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha

Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.

Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:

Moto: Kondoo, Simba,MshaleMaji: Ng’e, Samaki, KaaHewa: Mapacha, Mizani, NdooUdongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi

Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:

Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”:Kondoo, Kaa,Mizani,MbuziYenye Kubadilika “Mutable”: Ng’ombe, Simba, Ng’e na NdooIsiyobadilika “Fixed”: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki

 Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo

Alama ambayo ipo katika kundi la Udongona Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.

Haiba Na Tabia Za Alama Za Nyota

#1 Nyota Ya Kondoo: Machi 21 – Aprili 19

Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengineMwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juuAnauthubutu wa kujaribu mambo makubwaMwenzilishi wa mambo na mbunifuKiongoziMuongeajiNi mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.Mwaminifu kwa marafiki na familiaAnajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi

 #2

Nyota Ya Ng’ombe: Aprili 20 -Mei 20

Ni alama ya udongo:

Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakiliMakini na muangalifuAna kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisiMstahimilivuMwenye kutegemewaNi mgumu kubadilikaAnapenda vitu vizuri na vya thamaniUnapenda urembo na vitu vya kupendezaMwenye hisia zilizofichikaHuenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.

 #3 Nyota Ya Mapacha: Mei 21 – Juni 20

Ni alama ya hewa:

Ni mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaaAnafikiri kwa haraka na mcheshiNi mwasilianaji mzuriNi mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.Mwenye kuamua kwa akili na mbunifuHana utulivuAna mipango na malengo makubwaMwenye kubadilika kirahisi

#4 Nyota Ya Kaa: Juni 21 – Julai 22

Ni alama ya maji:

Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na amaniAnapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukooHisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikanaAna hurumaNi mwangalifuMkimya na

 #5  Nyota Ya Simba: Julai 23 – Agosti 22

Ni alama ya moto:

Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu.Anapenda kuonekana na watuSanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiweWana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwaNi viongozi wazuri na wenye nguvuMwenye matumaini mazuriMwenye kuheshimikaMshindaniMpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanyaMwenye mvuto

#6 Nyota Ya Mashuke: Agosti 23 – Septemba 22

Ni nyota yenye alama ya udongo

Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengineNi mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kaziniNi mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.Wapangili wazuri wa muda na watekelezajiNi mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.Wanajali afya

#7 Nyota Ya Mizani: Septemba 23 – Oktoba 22

Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.

Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.

Husimamia haki na usawaAnapenda sanaa na uremboWabunifu wa sanaaNi mpenzi wa muzikiNi muwazi katika kuonyesha upendoAna ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamiiAnatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisiaMpenda amaniWenye mvuto wa kupendwa

#8 Nyota Ya Ng’e: Oktoba 23 – Novemba 21

Ni alama ya nyota ya maji na ni mwenye hisia nzito

Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuriMjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwaAnapenda malumbano makaliWanatumia nguvuJasiriWastahimilivuWashindaniWanauwezo ,Wachunguzi wa mamboWasiriNi mpenzi mzuri na mwenye tabia za umilikiWanajitegemeaNi wenye maamuzi

#9 Nyota Ya Mshale: Novemba 22 – Desemba 21

Ni alama ya moto na ni mwenye mapenzi mazito na vitu

Mwanafalsafa na mkusanyaji wa habariMwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamotoNi mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.Ni mwenye kupenda uhuruNi mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wakeRafikiMwenye ariHawana utulivuWaaminifu na wakweliWanapenda safari

#10 Nyota Ya Mbuzi: Desemba 22 – Januari 19

Ni alama ya udongo na mwenye kuhitaji nyumba yenye amani ili kuhisi ukamilifu.

Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwaNi mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-MtendajiNi mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yakeSi mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maishaMgumu kubadilikaMbishi na asiyekubari kushindwa kirahisiMfanyabiasharaMwajibikaji

#11 Nyota Ya Ndoo: Januari 20 – Februari 18

Ni alama ya hewa:

Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.WakipekeeAnaejitegemea na hupenda kuwa peke yakeMwenye hurumaMuona mbaliMwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifuAnafanya marafiki wa aina mbalimbaliAna utu na mwenye kudai hakiAnapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa harakaAnapenda sanaa na maisha ya anasa.

#12 Nyota Ya Samaki: Februari 19 – Machi 20

Ni alama ya maji na ni mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo.

Ni mkweli na mwenye hisia nzitoHana ubinafsiNi mpenzi mwaminifu na rafikiMpenda amaniAna hurumaAnajitoaWana ndotoWabunifuWana aibu

Post a Comment

0 Comments