Kipigo cha Mtama Almaarufu kama Ngwara

 


MTAMA kwetu Lindi/Mtwara hutambulika kama Ngwara: sijui huko kwenu munauita vipi. Maana kuna mtama Manda (chakula) na Ngwara, Sasa hapa nazungumzia ule wa kupiga mtu. kama ule wa jana ule hahahaa

MTAMA Ni aina ya shambulio linalotumia mguu kumuangusha adui au yeyote uliyemdhamiria / unayepambana naye.


Mpigaji hudhamiria sehemu mbili au niseme kuna sehemu mbili zinazofaa kwenye kupiga mtama (Paja na sehemu ya nyuma ya ugoko Ambayo wataalamu huita CALF).


Kuna aina tatu maarufu za mitama.

 

1.Nje ya mguu 


2.Ndani ya mguu 


3.Shambulizi la kumalizia mguu uliosimama baada ya mguu mmoja kukamatwa. Mtama wa nguvu unaweza kukusababishia kukosa nguvu, kuyumba na kushindwa kusimama vizuri na wakati mwingine hukufanya ushindwe kutembea.


Ukirudia kupiga mtama kwa mara nyingi unaweza kuvunja au kuweka ufa kwenye mfupa, matatizo kwenye viungo vyaa mifupa (ligament na jointi) na matatizo kwenye misuli. Kwenye matukio ya kupigana mtama almaarufu Ngwara,neva ambayo ni ndefu kuliko neva zote mwilini mwa binadamu,


Kama una hamu ya kucheka, tazama au fuatilia pambano la Muhammad Ali na mjapani Antonio Inoki. Pambano lililopigwa baada ya Ali kujitapa kwa rais wa Japan. Na kusema yeyote atakayempiga jukwaani atampatia pesa za kutosha. Hii nitakupatia siku nyingine...


tumelizie Mtama wetu.

sciatic huathirika mara nyingi kwakua imetoka kuanzia sehemu ya chini ya uti wa mgongo, imepita kwenye kalio mpaka kwenye kisigino. Njia rahisi ya kukwepa mtama, inaitwa kitaalamu checking. Kabla mguu haujatua mwilini mwako, kwa haraka unauinua juu, hapo mpigaji anajikuta akipiga sehemu ngumu ya mguu wako na unaweza kumsababishia maumivu makali au hata kuvunja mguu wake. KESHO NANYOA NDEVU

Post a Comment

0 Comments