Siku njema ya kuzaliwa kwa @BillClinton, UJIO WAKE Tanzania na gumzo la chupa ya maji

 

Siku njema ya kuzaliwa kwa @BillClinton

SIJASOMA KITABU CHA MZEE MKAPA, ILA HILI SIDHANI KAMA HILI LIMEANDIKWA.

Twende pamoja kwa haya machache na mwisho uone mbwembwe za mwandishi wa habari huko AICC😄

Kama haujui, wanasema Bill Clinton ndiye rais mwenye IQ kubwa kuwahi kutokea nchini Marekani. Nianze kujitetea mapemaaaa , Me sio mtaalamu na sijui wanapima vp IQ, MACHACHE NI unaweza kujulikana kwa matokeo ya unachokifanya (darasani etc) au kwa unavyoishi… wataalamu watajazia


Wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi, vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 300,000. Ki historia sisi ni wapatanishi na hakuna atakayepinga hilio. mkutano wa upatanishi ulifanyika mkoani Arusha, Tanzania (Arusha Accords).

Wakiwa na lengo la kutuliza machafuko yaliyoanza chini kwa chini toka wakati wa uhuru hadi 1993 vuguvugu lilipobadilika na kuwa moto. Ona nataka kusimulia vita na lengo ni kumtakia siku njema ya kuzaliwa Rais mstaafu wa marekani Bill Clinton.


Bill Clinton akiwa na viongozi wengine 24 walifika Arusha kwa lengo la kuona vita vilivyopigwa miaka 7 vikiwa vinaisha. Na inasimuliwa siku hiyo wanajeshi na watu wa usalama kutoka Marekani walimwagika Arusha, ushawahi kuwaona FBI? WALE TUNAWAANGALIA KWENYE HOMELAND na Blacklist?


Basi unaambiwa walijaa Arusha hapo toooop.

Hata Nelson Mandela ambaye alikua baba mpatanishi, fimbo aliyoshikishwa na baba wa taifa wa Tanzania, hayati J.K.NYERERE alitua Arusha mida ya saa tatu asubuhi , tayari kwa kuanza kikao huko Arusha International Conference Centre, AICC




Siku hiyo Clinton alishuka maneno ya hekima sana. Nanukuu maneno machache


Mujitahidi mupate amani ili watoto wenu waweze kuisoma / kuitambua vizuri historia, na sio ninyi muwalazimishe kuirudia hiyo historia. Wanatakiwa waishi kwaajili ya kesho na sio hiyo jana yenu.


Munaweza kudhani nchi kama Marekani, inaweza kuwalazimisha mupatane lakini kupatana ni jambo la utayari baina yenu wenyewe.





Niishie hapo nisije kuwadanganya.


Kila mwandishi alitoka na ENGO yake siku hiyo. Twende kwa jamaa mmoja kutoka Kenya na gazeti lake la The Daily Nation

kama sikosei vile. Alisimulia vizuri ujio wa marais hawa kutoka sehemu mbalimbali. Mpaka pale alipoingia rais Mkapa na Clinton ambao walikaa sehemu ya pamoja. Anasema, marais waliwekewa maji pale mbele : maji ya chupa ya KILIMANJARO.


Nashukuru sipo chini ya taasisi wala kampuni , ndo natangaza biashara hivyo.

Rais mkapa akachukua maji yake na kunywa taratiiiiiibu… naye Clinton akatupa mkono wake kwenye chupa ya Kilimanjaro, kabla hajaigusa chupa , bodyguard wake akaiwahi ile chupa na kuyachukua yale maji, kwa haraka na ushupavu wa hali ya juu akambadilishia maji Clinton na kumpatia waliyotoka nayo nchini kwao.


Lilikua ni jambo dogo mno, lilionekana baada ya reporter huyu kuliandika. Sidhani ila nahisi ndio sababu ya mzee Mkapa kutembea na maji yake kutoka Tanzania, kila alipokua kwenye mkutano nje ya nchi baada ya mkutano ule wa Arusha.




Siku njema ya kuzaliwa bill Clinton na apumzike kwa amani mzee wetu mpendwa Benjamin .W. Mkapa.
























Post a Comment

0 Comments