Kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa Marehemu Langa, Wakazi Asimulia Kisa cha Shati Alilompatia

 


Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanamuziki wa mtindo wa rap wenye vionjo vya rege, Marehem Langa Kileo. Kama Langa angalikuwa hai, angalitimiza umri wa miaka 36 leo. Langa alifariki mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 28 tu, Malaria makali yalimchukua ndugu yetu..ama kweli Malaria haikubaliki.

Kupitia ukurasa wa twitter wa mwanamuziki Wakazi, ambaye hapo awali aliwahi kusoma shule moja na mwanamuziki Langa (Loyola Sec), anatusimulia ya kwamba, aliwahi kumpatia Langa shirt zuri ambalo alikuwa analipenda mno, kama zawadi kwa rafiki yake. Baada ya Langa kufariki, marafiki na watu wa karibu akiwemo wakazi, waliitwa ili wapatiwe vitu vya Langa....kwa bahati Wakazi akajikuta akipewa shati lile lile ambalo aliwahi kumpatia Langa akiwa hai. Stori imesisimua na kuibua hisia za watu wengi mno.



Kumbuka hapo awali, wakazi na Langa walifanya harakati za muziki wakiwa shuleni. Wakazi aliwahi kusimulia kuwa Langa alimtambulisha kwa kaka yake ambaye ni mtayarishaji wa muziki. Walitembeleana kama marafiki/Ndugu, Waliimba na kuchana pamoja lakini kabla shughuli ya muziki haijapikika kisawasawa baina yao, wakazi alikwenda Masomoni Nchini Marekani. Langa aliendelea na muziki hadi kupata fursa ya Cokacola Pop Stars, iliyoweza kumuibua yeye, Sara (SHAA) na Witness.



Licha ya kuwa mbali bado waliweza kuwasiliana. Wakazi alipokuja Tanzania alipata muda pia wa kumtembelea rafiki yake hadi pale kifo kilipomchukua.

Pumzika kwa amani Langa Kileo, tutakukumbuka kwa kujiamini hasa kwenye suala la Muziki

Post a Comment

0 Comments