Waziri Geoffrey Mwambe Ashauri Uwekezaji Kwenye Utalii Mkoani Lindi



Wananchi mkoani Lindi wameshauriwa kutumia fursa mbalimbali zilizomo mkoani Humo ili kujitengenezea kipato na ajira hasa katika suala la utalii.
Akizungumza baada ya kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii mkoani Lindi, waziri wa uwekezaji Geoffrey Mwambe amewataka wakazi wa mkoa huo pamoja na wafanyabishara kutoka sehemu mbalimbali, kuwekeza kwakuwa kumekuwa na vivutio vingi visivyotambulika kitaifa na duniani.

Mwambe anasema, kwa sasa wimbi la watu wengi mkoani Lindi na katika mikoa mingine ya jirani wamekuwa wakiusubiria kwa hamu mradi wa kuchakata Gesi asilia (LNG). Anasisitiza ya kuwa, endapo suala la utalii litatiliwa mkazo mkoani humo basi litapunguza idadi ya uhitaji kwakuwa kwa sasa watu wengi wamekuwa wakisubiri na wanategemea ajira kutoka katika mradi huo wa gesi.

Aidha, amepongeza Jitihada zinazofanywa na baadhi ya wawekezaji, kwani anaamini baada ya muda watanufaisha watu wengi mkoani Lindi na jitihada zao zitainufaisha serikali kwa kuleta wageni nchini na wawekezaji wakubwa.

Katika mahojiano, hakusita kutoa pongezi kwa uongozi wa Kuchele Beach, kwa kuandaa mambo mbalimbali yanayoitangaza mkoa wa Lindi na kufichua vivutio vya utalii kama mapango ya kale yenye historia ya kusisimua pamoja na utalii wa baharini (majini na nchi kavu).

Kupitia tamasha kubwa la utalii lililofanywa mkoani Lindi katika fukwe ya kuchele, ameomba liwe ni jambo linalofanyika mara kwa mara kwani linafungua milango mingi ya fursa na kuutangaza mkoa wa Lindi katika sekta ya utalii hasa wa fukwe na bahari.

Post a Comment

0 Comments