Wadau Walalamika Bei ya Vifaa vya Michezo kwa Wanafunzi Wenye Ulemavu

Wadau wa Michezo, Walimu na Wanafunzi Mkoani Lindi, wameiomba Serikali kushusha bei ama kufuta kabisa kodi ya vifaa vya michezo kwaajili ya watoto/wanafunzi wenye ulemavu ili kuweka haki sawa katika masuala ya Michezo na kuwapatia nafasi nzuri ya kushiriki kwenye Fursa mbalimbali za kimichezo.



Akizungumza wakati akikabidhi vifaa maalumu vya Michezo kwa wanafunzi wenye ulemu, Ramson Lucas ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi kutoka Sports Development Aid Mkoani Lindi, amekiri kutomudu gharama na kukidhi haja kwa wanafunzi wenye ulemavu katika kukabidhi vifaa hivyo kwani vimekuwa na gharama kubwa mno.



Anasema, ili wanafunzi wenye ulemavu waweze kushiriki katika michezo mashuleni ni lazima wapatiwe vifaa ambavyo kiuhalisia vimekuwa na bei ghali madukani.

Akizungumza kwa Niaba ya Afisa Elimu wa Mkoa katika hafla hiyo ya kupokea vifaa vya michezo kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu,  Afisa Elimu Taaluma Mkoani Lindi Kulwa James ameziomba taasisi mbalimbali za kiserikali na Binafsi kuwakumbuka watoto wenye ulemavu kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwani wamekuwa wakisahaulika mara nyingi hivyo misaada mingi imekuwa ikiwafikia wanafunzi wa kawaida.
"Wadau wengi katika eneo la michezo wanalisahau kundi la watoto maalumu, Hata kwenye UMISETA kundi hili halishirikishwi sana, Walau kwenye UMITASHUMTA tunawaona" Kulwa James



Nao walimu wamekiri kuwepo kwa uhaba wa vifaa vya michezo kwa wanafunzi wenye ulemavu huku wakisema pia, sababu nyingine ya Wanafunzi Maalumu kutoonekana wakishiriki michezo katika ngazi ya Sekondari ni kutokana na uchache wao kwani wazazi wengi wamekuwa wazito kuwafikisha watoto wao kupata elimu ya Sekondari na hivyo wengi huishia katika elimu ya Msingi, Anasema Mwalimu Shaibu Issa kutoka Halmashauri ya Mtama.



Kupitia Sports Development Aid mkoani Lindi, Ramson amekabidhi
Mpira Maalumu wa GoalBall Tsh 350,000
Mpira Maalumu wa Miguu Tsh 180,000
Jezi na vifaa vingine vyenye Tjamani ya shilingi Milioni tatu. Dhumuni ni kukabidhi walau kifaa kimoja kwa kila Halmashauri Mkoani Lindi.



Awali, Sports Development Aid iliweza kutoa Mipira 304 kwa mkoa wa Lindi kwaajili ya Michezo/Mashindano katika UMISETA na kwa shule zilizopo katika Mradi wao.


 







Post a Comment

0 Comments