Kwanini KANYE WEST aseme ana deni la dola million 53?

Mtandao wa TMZ umepata jibu la kwanini Kanye West alisema kuwa ana deni la dola milioni 53.
Umedai kuwa fedha hizo ni zile ambazo rapper huyo amewekeza kutoka mfukoni mwake katika miradi yake ya fashion na muziki.
Vyanzo vilivyo karibu na rapper huyo, vimeiambia TMZ kuwa fedha hizo ni pamoja na dola milioni 40 alizowekeza kwenye misimu mitatu ya nguo zake za Yeezy.
Pamoja na kwamba viatu vinamuingizia fedha zaidi, inasemekana kuwa kampuni ya Nike haikumpa hata senti pale alipotoa viatu vyake vya awali. Alivitengeneza viatu hivyo kwa hela kutoka kwenye mfuko wake mwenyewe.
Pia Kanye alitumia laki kadhaa kutengeneza sets za ziara yake iliyopita pamoja na filamu yake fupi ya mwaka 2012, Cruel Summer.
Habari njema kwa Kanye ni kuwa atarudisha fedha hizo kwakuwa mwaka 2015 pekee aliingiza dola milioni 22 na milioni 30 mwaka 2014, kwa mujibu wa Forbes.

Post a Comment

0 Comments