Nuh Mziwanda na shilole wapata wenza

Kama ulikuwa ni msiba wa ‘penzi’ basi arobaini imeisha na sasa maisha yanaendelea kwa wasanii wa Bongo fleva, Shilole na Nuh Mziwanda ambao uhusiano wao umekufa na kuzikwa kabisa.
Wiki chache baada ya couple ya ‘shiwanda’ kuvunjika, na juhudi za wadau mbalimbali kutaka kuwapatanisha kugonga mwamba (soma hapa ), inavyoonekana Nuh na Shishi kila mmoja ameamua kuendelea na maisha yake kwa kufungua ukurasa mpya wa mapenzi tena kwa vitabu tofauti.
Nedy Music
Shishi ndiye aliyeanza kuonesha dalili za kumpata mrithi wa Nuh, kwa kuanza kupost picha za msanii anayetumia jina la Nedy Music kwenye Instagram, na msanii huyo pia kupost picha tofauti tofauti za Shishi kwenye ukurasa wake.
Siku ya Valentine wawili hao walizidi kuthibitisha tetesi za uhusiano mpya kwa kupost picha wakiwa kimahaba zaidi kwenye kochi.

Post a Comment

0 Comments