Kijiji cha Bulongwa, wilayani Makete mkoani Njombe mwanaume anayetambulika kwa jina la Sylvester Mgowolwa amejinyonga baada ya kumyonga mchumba wake hadi kumuua.
Kahimu RPC Njombe SSP JohnTemu amedhibitisha kutokeea kwa tukio hilo. Kamanda Temu amesema kuwa Marehemu aliacha ujumbe kwamba sababu ya kujiua na kumuua mpenzi wake ni kwa kuwa alimsomesha chuo cha Nursing, akamfungulia duka la dawa baridi, na kumjemgea nyumba ya kuishi mjini Njombe.
Lakini baada ya muda mpenzi wake huyo akaanza kubadilika. Mgogoro huo ulikua mkubwa na mwanaume akaomba kuachana lakini kwa kugawana mali ambazo alimnunulia mchumba wake. Mchumba alikataa na ndipo kijana huyo alipoamua kumnyonga na kumuua kabla ya kujinyonga yeye mwenyewe.
#NB: Kuwa makini sn ktk kutafuta mwenzi wa maisha.!
0 Comments