historia ya osama bin laden Sehem ya 2

Baada ya kutembea na kuonana na wakimbizi pamoja na waathirika wa vita hivyo vilivyokuwa vimeletwa na majeshi ya Kisovieti Osama alirudi nyumbani yaani Saudi Arabia ili kuhamasisha michango pamoja na kuhamasisha vijana wa Kiarabu waliokuwa tayari kwenda Afgahanistan kuipigania ardhi yao. Alifanikiwa kuwarubuni waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya baba yake wenye asili ya Pakistan na Afghanistan na kuondoka nao kwenda Peshawar jimbo hili lipo nchini Pakistan) yalipokuwa makao yake kwa kipindi hicho. Alipofika Peshawar aliamu kujenga nyumba ya kufikia wageni (Guest House) iliyokuwa kiunganishi cha vijana wote waliokuwa wanataka kuingia vitani, ilikuwa ni nyumba nzuri iliyokuwa na huduma zote ikiwemo za utoaji wa habari, ilitumiwa pia na uongozi wa Mujahideen akiwemo na Abdullah Azam. Alijenga tabia ya kurudi Saudi Arabia kuhamasisha michango ya utu, kijeshi mara mbili kwa mwaka hadi mwaka 1982 aliposimama na kutorudi nchini kwake kwa mda mrefu.

Mwaka 1982 Osama Bin Laden aliamua kuhamishia makazi yake nchini Afghanistan na alikwenda na mashine zake nyingi za ujenzi na kuziweka kwenye maskani ya Mujahideen . Alianza kuutumia mda mwingi kwenye medani ya vita ila katika hali isiyokuwa na mpangilio wa kijeshi, kuonekana kwake katika uwanja wa mapambano kuliwatia sana moyo vijana wa Kisaudia waliokuwa vitani kwa uchache kipindi hicho na hivyo kuwafanya wengine waliokuwa hawajajiunga na vugu vugu hili la Mujahideen kujiunga nalo.

Osama aliendelea kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia wapiganaji wa Mujahideen ili kuyaondoa majeshi ya wavamizi (URUSI) kutoka kwenye ardhi ya Afghanistan. Katika kulifanikisha hilo alisaini mkataba wa siri na Rais Ronald Reagan wa Marekani pamoja na Viongozi wa CIA  mkataba uliomuwezesha yeye, Abdullah Yusuf pamoja na Mujehideen kupokea mamillioni ya fedha, vifaa vya kijeshi na misaada ya kiutu kutoka Marekani ili kusaidia kuyashinda majeshi ya Urusi.

Kufikia mwaka 1986 Osama Bin Laden alikuwa na makambi sita ya kukusanya na kufundisha vijana mafunzo ya kijeshi na hivyo kuweza kujitenga kutoka kwenye mafungamano na Mujahideen na kuweza kusimama mwenyewe kwenye medani ya vita nchini Afghanistan kwa kutumia kamandi zake mwenyewe. Kujitenga huko hakukumfanya kuwa adui wa viongozi wa Mujehideen au Abdullah Azzam laah hasha ila kulifanywa kwa mbinu ya kuweza kuongeza ufanisi kwenye medani ya vita, wengi wanadai kuwa huu ulikuwa ni ushauri aliopewa na CIA ili kuweza kusaidia kuongeza ufanisi wa kivita.  Naomba ifahamike kuwa katika kipindi chote hicho cha vita  Marekani na washirika wake walikuwa wakimuita OSAMA na wapiganaji wake kwa jina la WAPIGANIA UHURU (Freedom Fighters).
Mwaka 1986 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa Osama maana ndio mwaka aliyoweza kuanzisha ya moja kwa moja na majeshi ya Kisovieti kwa kutumia kamandi zake mwenyewe. Katika moja ya pambano kubwa ambalo alifanikiwa kuyarudisha nyuma majeshi ya Kisovieti ni lile la Jaji katika jimbo la Baktia.

Mwaka 1988 aligundua kuwa alikuwa nyuma sana kwenye kutoa maelezo kwa ndugu na jamaa wa vijana waliokwenda Afghanistan kupigana pamoja nae na hivyo aliamua kuwa na mfumo maalum na wa kisasa kwa ajili ya kuwatambua wageni wote waliokuwa wanaingia kwenye vikosi vyake. Mienendo yao ilikuwa ikirekodiwa kuanzia walivokuwa wanaingia Peshawar kwenye ile nyumba ya wageni alioijenga hadi kwenye makambi ya mafunzo. Mzunguko huu wote ulipewa jina la Al-Qa'edah  neno lenye maana ya kituo cha Kijeshi kwa lugha ya Kiswahili.

OSAMA ARUDI NYUMBANI

Mwaka 1989 majeshi ya Kisoviet yalishinwa vibaya kwenye vita nchin Afghanistan na hivyo Osama aliamua kurudi Nyumbani Saudi Arabia kwenye safari ya kawaida. Huko alizuiliwa kusafiri nje ya nchi na kuanza kufuatiliwa na utawala wa kifalme wa nchi hiyo. Lengo kubwa la kumzuia kusafiri nje ya Saudi laweza kuwa kwa sababu aliyashinda majeshi ya Kisovieti ila kubwa zaidi lilikuwa kwa sababu alihusishwa na kutaka kuanzisha Jihadi mpya Kusini mwa Nchi ya Yemen. Aliuzodoa Uongozi wa Kifalme wan chi hiyo ya Saudi kwa kumkumbatia Saddam Hussein aliyeonekana kutaka kuivamia Kuwait na hata kuweza kusonga mbele kuivamia nchi hiyo takatifu ya Saudi Arabia. Alionywa mara kadhaa kukaa kimya na kutotoa mihadhara ila hakusikia. Kwa kipindi hicho ufalme wa Saudi ulikuwa na mahusiano mazuri sana na utawala wa Saddam Hussein. Pamoja na kuwa zuio la kutosafiri nje ya nchi ial hakukosa uhuru wa kiasi cha kutoongea na kutoa maoni yake. Aliandika barua ya siri  kwa Ufalme wa Saudi iliyokuwa na ushauri wa kijeshi, kitaalamu jinsi ya kuweza kuyashinda majeshi ya Saddam endapo yatajaribu kusonga mbele kujaribu kuivamia ardhi ya Saudi.

Post a Comment

0 Comments