Osama bin Laden alizaliwa tarehe 10 March, 1957 mjini Riyadhi nchini Saudi Arabia. Ni motto wa 17 kati ya watoto 52 wa Billionea Mohammed bin Awad bin Laden. Baba yake alikuwa tajiri mkubwa nchini Saudi Arabia mwenye asili ya Yemeni aliehamia nchini humo, kaka na dada zake Osama walipata elimu zao katika nchi za Magharibi na baada ya kumaliza walirudi kufanya kazi katika kampuni la baba yao lakini Osama alisoma karibu na nyumbani na alipofika umri wa miaka 17 alimuoa Najwa Ghanem huko Latakia, Syria na kama ilivyokuwa kwa vijana wengi wa Kisaudia Osama alijiunga na kikundi cha Islamist Muslim Brotherhood.
Majina yake kamili ni Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden. Baba yake alimtariki mama yake mapema baada ya Osama kuzaliwa. Osama alikuzwa na kulelewa katika madhehebu ya Kislamu ya SUNNI.
Osama Bin Laden alipata shahada yake ya Uchumi na Biashara ya Chuo Kikuu cha Mfalme Abduaziz mwaka 1979. Vyanzo vingine vinadai kuwa Osama aliwahi kusoma shahada ya kwanza ya kwanza ya Uhandisi wa Ujenzi. Vyanzo vingine vinadai kuwa Osama alikatisha masomo yake ya Chuo Kiku akiwa mwaka wa tatu. Waliosoma nae wanamtaja kuwa ni mtu aliekuwa anajituma sana katika kazi zake na asiekata tamaa. Alivyokuwa chuo kikuu alipendelea sana masomo ya dini na aliutumia mda mwingi kutafsiri Quran na Jihad na alipenda sana kufanya kazi za kujitolea ikiwemo na kuwasaidia maskini. Pia alikuwa ni mpenzi mkubwa wa uandishi wa Mashairi na msomaji wa mashairi pia. Pia alikuwa mpenzi na mfuatiliaji wa kazi za Field Marshal Bernard Montgomery na Charles de Gaulle, Osama alikuwa mpenzi mkubwa wa michezo na alipenda sana kucheza mchezo wa soka , katika mchezo wa soka Osama alikuwa anacheza katika nafasi ya mshambuliaji wa kati na alikuwa shabiki wa klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza.
MAISHA YA NDOA YA OSAMA BIN LADEN
Kama nilivyotangulia kusema hapo juu alipofikisha umri wa miaka 17 aliingia kwenye ndoa, hiyo ilikuwa mwaka 1974, alidumu na huyo mke wake wa kwanza hadi mwanzoni mwa miak ya 2000 alipomtariki, wake wengine wa Osama ni Khadijah Sharif aliyemuoa mwaka 1983 na kumtariki miaka ya 1990, mwingine ni Khairiah Sabar aliyemuoa mwaka 1985 na Siham Sabar aliyemuoa maka 1987 na mwingine ni Amal al-Sadah aliyemuoa mwaka 2000. Osama anakadiriwa kuwa na watoto kati ya 20 hadi 26. Watu wa karibu na Osama ikiwemo walinzi wake wanamuelezea Osama kama baba bora wa familia aliependa kuwa mfano kwa wanae na familia yake nzima, hakupenda mchezo na ujinga kwa wanae. Alipenda kuichukua familia yake na kutoka nae kwenda jangwani ufanya mazoezi ya kulenga shabaha pamoja na kufurahi.
1979 YABADILI USO WA OSAMA BINI LADEN
Baada ya kumaliza/kuacha chuo mwaka 1979 Osama alienda Pakistan kujiunga na Abdullah Azam mhubiri wa Kiislam aliekuwa akimhusudu sana tokea akiwa mdogo na wakati akiwa chuoni. Mhubiri huyu alikuwa muumini mkubwa wa Jihad na alieamini kuwa Nchi za Kiislam zapaswa kuwa dola moja linaloendeshwa kwa sharia na misingi ya kidini. Ikumbukwe kuwa mwaka 1979 majeshi ya Kisoviet ya Urusi yaliivamia ardhi ya nchi ya Afghanistan na huo ndio ulikuwa mwanzo wa Osama Bin Laden kuonesha msimamo na imani yake kwa watu waliokuwa wananyanyasika na mauaji ya majeshi hayo ya Urusi. Akiwa nchini Pakistan yeye na Abdullah Yusuf Azzam waliendesha kampeni kabambe a kuwasaidia watu wa Afghanistan, ikiwemo michango ya fedha, silaha, vyakula na pia waliwakusanya vijana kwa ajili ya kuwafundisha kupigana. Osama alitumia sehemu kubwa ya utajiri wake kuwasaidia vijana wa Mujahideen waliokuwa mstari wa mbele kupigana na majeshi ya wavamizi, aliweza kuhamasisha vijana wengi kutoka mataifa yote ya Uarabuni kujiunga na Mujahideen ili kuweza kuyaondoa majeshi ya Urusi kwenye ardhiyao, katika uhamasishaji huo alitengeza makambi ya mafunzo kwa ajili yao. Pia ifahamike kuwa kwa mda wote huo Marekani na Saudi Arabia zilikuwa zinatoa misaada yote ya kijeshi, kifesha, vyakula kwa ajili ya vijana wote waliokuwa wanafundishwa kwa ajili ya vita. Nchi ya Pakistani ilichukua mamuzi ya kuwapa mafunzo ya kijeshi vijana hao na wengine walikuwa wakifundishwa na kambi za Osama Bin Laden akisaidiana na Mwalimu wake Abdullah Yusuf Azzam lakini kwa kiasi kikubwa kipokea msaada wa kifedha kutoka Saudi Arabia na Marekani pamoja na kutumia utajiri wake pia. Naomba ifahamike kuwa Osama alikuwa na utajiri unaokadiriwa kuwa kati ya Dollar za Kimarekani 25 hadi 30 kwa miaka hiyo ya mwanzo ya 1980, ni urithi alioupata kutoka kwa baba yake mzazi.
ITAENDELEA……….
0 Comments