Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba kuanzia leo
atakua mikononi mwa Sony Music kuanzia leo,
kampuni kubwa ya muziki inayofanya kazi na
mastaa wa dunia kama Beyonce , John Legend na
Chris Brown.
Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza
Alikiba kweye kiwango cha juu zaidi kimuziki,
kibiashara na kugharamia video zake na
anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya
unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music
kwenye masoko makubwa ya muziki kama
Marekani , Ulaya na Africa.
Sio kila msanii wa Afrika ameweza kusaini na Sony
Music ambapo nimeambiwa kwenye shughuli hii ya
leo kwamba mkataba aliosaini Alikiba unafanana
kabisa na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria
Davido ambapo unavipengele vya kusababisha
kolabo kwa urahisi zaidi na mastaa wakubwa
wakiwemo wa Marekani.
0 Comments