Leonardo Da Vinci (Vinci,Toscana, Italia, 15 Aprili 1452 –Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwamtu mwenye vipaji vingivingi kutoka italy
Kifupi, alikuwa mwanahisabati,mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi,mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji,msanifu majengo, mwanabotania,mwanamuziki na mwandishi.
Ndiye mwakilishi bora wa tapo laRenaissance.
Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.
Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa nashauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".
Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.
Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli,kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuzanishati ya jua kuwa umeme.
Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani niMona Lisa na Karamu ya mwisho.
Mchoro mwingine unaojulikana sana niVitruvian Man. Unajulikana sana hataHomer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.
Maisha
Utoto, 1452–1466
Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili1452, mkoani Toscana, katika mji mdogo wa kilimani wa Vinci, katika mabonde ya Mto Arno, karibu naFlorence nchini Italia.
Babu yake, Ser Antonio, anajivunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwahawajaoana. Baba yake alikuwamwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci. Mama yake, Caterina, alikuwa mhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutokaMashariki ya Kati. Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".
Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba yashambani na mama yake. Halafu akaja kuishi Vinci na baba yake, mkewa baba yake aliyeitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco.
Wakati Leonardo ameshakua, aliandika vitu viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitandachake cha watoto nje ya nyumba yaondege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikiayake ikawa inamfutafuta sura yake.Kumbukumbu nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligundua pangomilimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa nakiumbe kikubwa cha ajabu kimejificha mle ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua kilichopo mle ndani.
Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifochake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu utundu aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiuza kwa wauzaji wabidhaa za kisanaa.
Ujana na utu uzima
Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Alifunzwa usanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio.
Sehemu kubwa ya maisha yake alimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Italia.
Mwaka 1516 Leonardo alikwendaAmboise, Ufaransa, baada ya kupatamwaliko kutoka kwa mfalme Fransisko I. Kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu waMonalisa.
Leonardo aliishi mjini Amboise, katikanyumba yake nzuri aliyopewa naMfalme huyo wa Ufaransa, miaka yake ya mwisho, toka mwaka huo mpaka mwaka 1519.
Afya yake haikuwa nzuri kwa sababu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517, lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.
Kifo
Alifariki huko Amboise tarehe 2 Mei 1519 akiwa na umri wa miaka 67, akazikwa St. Hubert.
0 Comments