Mjue MOBUTU SESE SEKO

Joseph-Désiré Mobutu aliyejiita baadaye Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga (* 14 Oktoba 1930 Lisala; † 7 Septemba 1997Rabat - Moroko) alikuwa rais nadikteta wa Zaire (Kongo-Kinshasa) kati ya 1965 na 1997.

Utoto na jeshi la kikoloni

Alizaliwa katika Kongo ya Belgijimwaka 1930. Kijana baada ya shule alijiunga na "Force Publique" yaani jeshi la kikoloni la Wabelgiji katika Kongo. Hadi 1956 akafikia cheo cha staff sajent akaacha jeshi na kufanya kazi magazetini akashiriki katika siasa.

Kupanda ngazi

Baada ya uhuru wa Kongo serikali ilimpa cheo cha kanali akawa jeshi mkuu wa Kongo. Katika nafasi kama mkuu wa jeshi alishirikiana na raisJoseph Kasavubu katika uasi dhidi ya waziri mkuu wa kwanza Patrice Lumumba aliyepinduliwa tar 14 Septemba 1960 na kuuawa baadaye.

Raisi wa kijeshi

Mwaka 1965 Mobutu aliamua kumpindua Kasavubu akachukua uraisi mwenyewe. 1970 alijirudisha ofisini kwa njia ya uchaguzi uliopangwa naye wenyewe. 1969 alikandamiza upinzani wa wanafunzi wa chuo kikuu kwa nguvi ya kijeshi. Baada ya kuua wanafunzi wengi aliamuru 2000 wengine waingie katika jeshi ili wajifunze nidhamu.

Mapinduzi ya utamaduni wa Kiafrika

1970/1971 Mobutu alitangaza kile alichoita "kempeni ya utamaduni wa Kiafrika". Alibadilisha jina la Kongo kuwa Zaire na raia wote waliagizwa kuacha majina yao ya Kikristo yenye asili ya Ulaya na kutumia majina ya asili ya Kiafrika. Suti za kiulaya zilipigwa marufuku na rais mwenyewe alianza kuvaa suti zilizoiga mfano wa Mao-Tse-Tung.

Mobuto mwenyewe alianza kujiita "Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga" yaani "Shujaa mwenye enzi asiyeshindikana". Kiuchumi alitaifisha makampuni ya kimataifa mara nyingi kwa kuzikabidhi kwa ndugu na wenzake. Lakini hadi 1977 hali ya uchumi ulizorota kiasi cha kumlazimisha kuwaomba wageni warudi tena.

Raisi mwizi

Chini ya Mobutu nchi kubwa ya Kongo-Zaire ilirudi nyuma. Mobutu alijitajirisha kupita kiasi wakati nchi yake ilioza. Mwaka 1984 mali yake ya binafsi nje ya Kongo ilikadiriwa kuwa dolar za Marekani bilioni 4. Nchi kubwa za Magharibi kama vile Marekani naUfaransa walimvumulia na kumsaidia kwa sababu alionekana kama mwanasiasa anayesaidia kupambana na ukomunisti na harakati za ukombozi kwa mfano Angola.

Wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi za magharibi hawakuona haja tena kumsaidia Mobuto. Tangu 1990 alipaswa kukubali vyama vya upinzani hata akijaribu kuendeleza udikteta wake.

Upinzani na mwisho

Katika miaka ya 1996 na 1997 waasi waliongozwa na Laurent Kabilawalienea katika mashariki ya Zaire kwa msaada wa nchi jirani Uganda naRwanda. Mobutu alipaswa kumkubali mpinzani wake Etienne Tshisekedikama waziri mkuu lakini jeshi la Kabila likaendelea kusogea mbele. Tar. 16 Mei 1997 wapinzani walitwaa uwanja wa ndege wa Lubumbashi na Mobutu aliyegonjeka alikimbia nchi. Alikufa nje nchini huko Moroko 7 Septemba1997. Kabila alikuwa ameshaingia tayari Kinshasa tangu 20 Mei 1997 na kuchukua utawala.

Post a Comment

0 Comments