Mjue William Shakespear

William Shakespeare (Aprili 1564 - 23 Aprili 1616) alikuwa mwandishimashuhuri nchini Uingereza.

William Shakespeare

Waingereza mara nyingi humtazama kuwa mwandishi mkuu wa lugha yao. Aliandika hasa maigizo na tamthiliya. Alifanya pia kaziya uigizaji.

Mwandishi huyo akiwa mdogo alikuwa anapenda kusoma sana hadithi mbalimbali ambazo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha yaKilatini. Shakespear alisoma zaidi kazi zawanafalsafa wakongwe wa Kigiriki Aristotlena Plato, pia alipenda sana teolojia.

Maigizo yake hupangwa katika vikundi vya:

mchezo tanziatamthiliya ya kuchekeshatamthiliya ya kihistoria

Kutokana na wingi wa kazi na mada, wataalamu wengine hawakubali ya kwamba maandiko yote yanayojulikana kama ya "Shakespear" yameandikwa na mtu yeye yule, lakini walio wengi wameridhika ya kwamba huyu Shekespear wa kihistoria mwenyewe alikuwa mwandishi wa hayo yote.

Tamthiliya zake

Kati ya maandiko yake mashuhuri ni:

Michezo TanziaRomeo and JulietMacbethKing LearHamletOthelloTitus AndronicusJulius CaesarAntony and CleopatraCoriolanusTroilus and CressidaTimon of AthensTamthiliya za KuchekeshaThe Comedy of ErrorsAll's Well That Ends WellAs You Like ItA Midsummer Night's DreamMuch Ado About NothingMeasure for MeasureThe TempestTaming of the ShrewTwelfth Night or What You WillThe Merchant of VeniceThe Merry Wives of WindsorLove's Labour's LostThe Two Gentlemen of VeronaPericles Prince of TyreCymbelineThe Winter's TaleTamthiliya za KihistoriaRichard IIIRichard IIHenry VI, part 1Henry VI, part 2Henry VI, part 3Henry VHenry IV, part 1Henry IV, part 2Henry VIIIKing John

Mchezo tanzia "Julius Caesar" pamoja na tamthiliya ya kuchekesha "The Merchant of Venice" vimetafsiriwa na Mwalimu Julius Nyerere kwa lugha ya Kiswahili ("Julius Kaisari" na "Mabepari wa Venisi")

Post a Comment

0 Comments