Ampa mkewe ujane akiwa na miaka 27 sababu ya dawa za kuongeza nguvu za kiume

MSIMULIAJI KUTOKA J.F:
Kama kichwa kinavyojieleza, hii imetokea karibuni
kwa rafiki yangu aliekaa kwenye ndoa yake ya
isiyozidi miaka 5 iliyokatishwa na dawa za kuongeza
nguvu za kiume alizotumia mumewe.
Siku ya tukio:
Nakumbuka Hiyo siku nikiwa kazini asubuhi
nilipokea simu ya rafiki yangu akinambia mumewe
ameugua ghafla asubuhi na mda huo
wamemkimbiza hosp moja maeneo ya jirani lakini
tayari hawezi kuongea wala kufumbua macho,
madaktari bado wanaeendelea na vipimo.
Baadae ikabainika kuwa mgonjwa presha yake iko
juu sana hivyo walikuwa wakipambana kuishusha ili
apate fahamu, lakini mpaka inafika mchana zoezi
halikufanikiwa hivyo madaktari walilazimika kutoa
transfer apelekwe Muhimbili, rafiki yangu
alivyonipa taarifa kuwa wanaelekea Muhimbili
ilinibidi nitoke kazini ili tuwe wote huko Muhimbili.
Nilipofika wao tayari walikuwa kitengo cha
emergency kwa ajili ya check up mbalimbali
nakumbuka tulikaa pale mpaka saa tano usiku
daktari akasema mgonjwa hali yake mbaya sana
inawezekana presha imepelekea mshipa wa damu
kichwani kupasuka lakini hatuwezi kusema moja kwa
moja mpaka tumfanyie scan ya kichwa ambayo
hawezi kufanyiwa akiwa hana fahamu inabidi
waendelee kushusha presha wakati wanasubiri
apate fahamu waweze kumfanyia hicho kipimo
ikabidi mgonjwa apelekwe ICU nasi tukaambiwa
tuondoke turudi asubuhi
Ikawa zoezi letu ni kwenda Muhimbili lakini hakuna
mabadiliko, presha ilishuka lakini mgonjwa haamki
mpaka alipotuacha baada ya siku ya 3.
Kwanini nimesema alitumia dawa za kuongeza
nguvu:
Juzi wakati nimekaa na mjane tukajikuta
tunaongelea tena suala la marehemu mumewe,
akawa ananambia anahisi mume huyo alitumia dawa
za kuongeza nguvu maana ile siku ya tukio jana
yake wakati wanakutana kimwili alikuwa na spidi
isiyo kawaida na walifanya kwa mda mrefu tofauti
na siku zote na bado asubuhi wakaendelea na
walipomaliza ile round ya asubuhi mumewe akaanza
kujisikia vibaya ghafla alipojaribu kuamka ndipo
kuanguka na baada ya mda kuanza kutapika
nyongo.
Pia madaktari wa hospitali zote mbili walikuwa
wakimuhoji mke endapo anafahamu kama mumewe
amekuwa akitumia dawa zozote za kuongeza nguvu,
walimuuliza ivyo kutokana na mazingira ya tukio
lilivyotokea lakin alikataa sababu hakuwai kumuona
lakini madaktari wakamwambia inawezekana kwa
98% mume alitumia vidonge hivyo na ndio
vilivyopelekea kupandisha presha kwa kasi.

Post a Comment

0 Comments