Na Humphrey Moris
Waandishi wengi wa habari wanafeli kwa asilimia kubwa kuripoti na kuandika habari za jamii, zaidi katika kuonyesha maovu ili kuleta mabadiliko. Simaanishi kila muandishi anatakiwa kuripoti negative (Kukosoa tu) ,HAPANA. Lakini wananchi wanachoka na sifa zisizo na tija wakati matatizo ni mengi.
Waandishi wamenunuliwa na vyama na wakuu wa
serikali. Kwa mfano, unakuta muandishi wa kituo Fulani cha habari,kila siku na
kila muda yupo mgongoni mwa kiongozi (UTADHANI NI MWANDISHI WAKE). Waandishi
wamekua maarufu katika kuripoti matamko ya viongozi au uzinduzi. Kwani taaluma
yenu inawaambia hao ndio wenye habari pekeyao? Unakuta habari ya siku moja
inakatwa vipande vipande ili kupata habari na matukio ya wiki nzima.
Mnasahau huku mtaani kuna matukio na visa
vingi ambavyo vinaleta habari pia. Hii haita taarifu tu bali italeta mabadiliko
pia kwa wananchi hao. Kuna umuhimu gani wa kwenda kwa mkuu wa mkoa kuuliza kama
kuna lolote litakalokupa habari wakati kuna UVUNJWAJI WA HAKI ZA BINADAMU.
MANYANYASO NA UONEVU KWA KINA MAMA. Huko kwa wakuu kuna nini zaidi
linalowafanya mugande kwao tu?
Wananchi wanashangazwa na habari ambazo
hawajui kama zimejiri kutoka mikoani mwao.Sijui zinatengenezwa? . Kwa maana kawaida
wananchi ushuhudia tukio mchana na jioni hukaa kwa pamoja wakisubiri kuona
kilichojiri mchana katika televisheni au kusikika kwenye redio, Na wakibahatika
kuona ufurahi kwakua wanadhani jambo lao limesikika na litatatuliwa .SIKUHIZI HAKUNA HII. Habari
zinazosikika siku hizi ni MKUU WA MKOA AFANYA MAZOEZI NA WAFANYAKAZI WA OFISI
FULANI. MKURUGENZI APOKEA ZAWADI FULANI KUTOKA KWA KAMPUNI FULANI. MKUU AZINDUA
CHOO. Ya wananchi tunayaacha yakibembea mitini.
Siku kadhaa zilizopita, nilibahatika
kutembelea kata 10 zilizopo wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma. Kwa kile
kilichotupeleka katani humo na tuliweza kupata visa na malalamiko kutoka kwa
wananchi. Hapa nilijiuliza kama kweli tuna waandishi wa habari?. Nilipata mambo
mengi mapya na yenyekusisimua yanayowasibu wananchi.
1; Wananchi wanakero za kudhulumiwa na watu
wanaojifanya wanatoka serikalini. Kwa mfano , kuwaamrisha waandae vikundi ili
waweze kupata mkopo huku wakiwachangisha pesa na kukimbia nazo.
2; Rushwa imekithiri. Kuna matukio mengi
yanayohusisha masuala ya rushwa kwa wananchi
a.
Ili wapate
haki zao kama mahospitalini
b.
Kushawishiwa
ili kuepuka adhabu kubwa hasa na maaskari
3; Malalamiko juu ya miundombinu mibovu kama
barabara na ukosefu wa maji
4; Malalamiko ya wananchi kwa serikali yao. Kwa
mfano upishaji wa ujenzi wa vitu vya serikali na barabara bila malipo. Wananchi
wanalalamika
Kuna mambo mengi sana ambayo waandishi
walipaswa wayaweke wazi. Lakini waandishi wanakesha maofisini na kuwa kama
mikia migongoni mwa viongozi.
Wengi wao ukiwauliza wanajibu kwa mzaha kuwa WANANCHI WA KAWAIDA HAWATOI POSHO ila
maofisini posho nje nje.( WAANDISHI MUNASIKITISHA MNO)
TATIZO NI NINI?
UMASIKINI
AU NJAA? Labda viongozi
wanawapa kitu kidogo ndio maana hamukauki huko maofisini.
AU
NI WAOGA? Labda munaogopa
kuripoti ya wananchi kwakua munahisi yatagusa vitu Fulani . lakini mkumbuke kazi
ya uandishi inaendana na kiapo cha kujitoa kwa lolote ilimradi uweze kufichua
uozo. Kama hautaweza kujitoa basi taaluma hii haikufai.
ASILI
YA VYOMBO VYA HABARI NA MAMENEJA? Labda mabosi wenu wameridhika na habari zenu nyepesi zilizojaa ukasuku
na kuwasahau wananchi. AU MULIJISAHAU?
WAANDISHI
MMELALA HAMUONEKANI
Habari zetu nzito zinaripotiwa na vyombo vya
habari vya nje kwa mfano BBC. Tunatambua record mbali mbali za watu ,kama wazee
wenye umri mkubwa baada ya vifo vyao na si kabla.Walau tungeonekana kuwa nasi
tunaye mtu mwenye umri mkubwa zaidi ya wote DUNIANI. Siamini kama mtu mwenye
mbio nchini kwetu wa mwisho kutokea ni Filbert Bahi tu waandishi tembeleeni
vijijini na sehemu mbalimbali mupate kuona mengi na muifumbue dunia macho. Sisi
wenyewe tumeduwaa kama samaki kwenye
vikaango. Tukinong’ona kama mjadala wa panya kumfunga paka kengele kati yetu
nani atafanya.
WAANDISHI
TEMBEENI ACHENI KUKAA KWENYE OFISI ZA VIONGOZI KUSUBIRI HABARI.
Tunawasikia tu mukilalamika taaluma yenu
imeingiliwa na baadhi ya watu fulani mitandaoni. Watu wasio hata na robo ya
ujuzi wa masuala ya habari, wamechukua nafasi na kuwahabarisha wananchi mambo
nyeti yanayohusu jamii. Ila watu hawa kwa muda mwingine hukosa maadili ya
uandishi na hii inapelekea waandishi wote waonekane ni sifuri.
TAALUMA
INADHARAULIWA SASA
Kuonekana kwa waandishi ni sifuri, tunaona
sasa wamiliki wa vyombo vya habari wameamua kuajiri watu maarufu (Celebs). Msanii
wa muziki si ajabu ukamkuta kwenye tv au radio akitangaza WAANDISHI ZIRO
WAMEPIGWA KNOCK OUT. MUSILALAMIKE NI NYINYI MUMETAKA KUONEKANA WA KAWAIDA
KATIKA TASNIA HII. Ninyi si mumeamua kua waandishi wa vyombo vya maofisini.
EMAIL ; Morisehumphrey@yahoo.com
# 0625773039
0 Comments