Baada ya kumueleza hivyo kimya kimya
akamuamuru muhudumu huyo akae karibu nae na
kuanza kumpa maagizo. Lakini kabla ya hapo yule
mhudumu akataka ampe uhakika kama kweli ana
bomu. Cooper akachukua briefcase yake na
kuifungua kidogo tu ili muhudumu aangalie na
alipoangalia ndani ya briefcase akaona cylinders
nane, nne zikiwa chini na nne zikiwa juu zikiwa
zimeunganishwa kwa nyaya nyekundu ambazo nazo
zinaenda kuunganika kwenye battery yenye rangi
nyekundu pia ikiyopo pembezoni mwa briefcase.
Baada ya kuchungulia muhudumu akaamini kweli
Cooper alikuwa na Bomu.
Cooper akampa maagizo muhudumu akaongee na
marubani kwa kupitia intercom kuwa wawasiliane na
uwanja wa ndege wa Seattle na wawaeleze juu ya
ndege kutekwa na mtu mwenye bomu na yuko
tayari kulipua ndege hiyo na abiria wote 36 na
watumishi wa ndege 6 waliopo umo ndani.. (Ndege
ilikuwa haijajaa yote, ilijaa kama theluthi moja tu
(1/3)).
Ili asilipue ndege hiyo Cooper alihitaji apewe 'Fedha
halali za kimarekani' dola 200,000 (msemo huu
'fedha halali za kimarekani' utakuja kuleta maana
sana huko mbele kwenye upelelzi wa FBI). Pia
aliamuru apewe parashuti nne na ndege itakapofika
uwanja wa ndege wa Seattle kuwe na gari ya kujaza
mafuta inasubiri ili ijaze ndege mafuta na
kumpeleka sehemu atayoitaka.
Muhudumu Bi. Schaffner akawasiliana na mapilot na
kuwahakikishia kuwa ni kweli jamaa ana bomu na
akawapa orodha ya vitu alivyokuwa anavitaka.
Baada ya kupewa orodha ya demands za Bwana
Cooper, marubani wakawasiliana na uwanja wa
ndege wa Seattle na watu wa uwanja wa ndege
wakawasiliana na vyombo vya ulinzi na baada ya
mtiririko wa mawasiliano kati ya uwanja wa ndege,
wamiliki wa ndege na vyombo vya ulinzi kufanyika
wakakubaliana kuwa ili kuepusha hasara ya
kibiashara na kupoteza maisha ya watu 42 ni vyema
wakampatia mtekaji anavyovitaka lakini vyombo vya
ulinzi vitaangalia kama kutapatikana fursa yoyote
waweze kumkata au kumdungua mtekaji huyo.
Hivyo basi wahudumu wote waliopo kwenye ndege
waliamuliwa wampe ushiriakiano Cooper ili kuepusha
hatari yoyote na pia wamueleze kuwa awape mda
kidogo ili kukamilisha kupata vitu alivyokuwa
anavihitaji.
Baada ya jibu hilo kurudishwa juu kwenye ndege na
marubani kuwasiliana na muhudumu Schaffner
kupitia intercom, muhudumu alirudi kwenye siti
aliyokaa Cooper na alikuta sasa amevaa miwani
meusi ya jua na yuko amerelax kabisa bila presha
wala wasiwasi wowote! Akampatia jibu walilopewa
kutoka chini kwenye uwanja wa ndege.
Baada ya kupewa jibu hilo Cooper akaitikia kwa
kichwa kisha akawasha sigara nyingine na kuagiza
Soda nyingine na maji ya kunywa, na kwa mshangao
akalipia na chenji iliyorudi akampa 'tip' muhudumu
Schaffner.
Muda wote huu abiria wengine walikuwa hawajui
kinachoendelea ndani ya ndege na ili kuepusha
wasije wakapata wasiwasi kutokana na kuchelewa
kutua wakatangaziwa kuwa kulikuwa na tatizo la
kiufundi hivyo itawalazimu wachelewe kutua mpaka
tatizo litakapo shughulikiwa.
Kama nilivyoeleza awali kutoka Portland mpaka
Seattle ni safari ya nusu saa kwa ndege lakini
ndege ilikaa angani taribani masaa mawili ikiwa
inazunguka tu ili kusubiria kule chini mamlaka usika
ziandae vitu cooper alivyohitaji.
Ndani ya masaa mawili FBI walifanikiwa kukusanya
noti za dola 20 zipatazo elfu kumi (jumla dola
200,000) kutoka bank za karibu na zote wakazipiga
picha! Pia walifanikiwa kupata parashuti nne kutoka
katika kituo cha jeshi la anga cha Tacoma kilichopo
karibu na uwanja wa ndege wa Seattle! Baada ya
kumaliza kufanya maandalizi yote haya mnamo
majira ya saa kumi na moja dakika ishirini na nne
wakawasiliana na ndege juu kumtaarifu Cooper
kuwa vitu vyake vyote alivyohitaji viko tayari.
Baada kumpa orodha ya vitu hivyo Cooper akaamuru
kuwa hataki parashuti za kijeshi anataka apewe
parashuti za kawaida za kiraia na FBI wakafanikiwa
kuzipata kutoka katika kituo cha kufunza watu
skydiving.
Robo saa baadae (saa kumi na moja dakika 39)
ndege ilitua katika uwanja wa Seattle na Cooper
akamuamuru rubani aisimamishe ndege sehemu
pweke na yenye mwanga wa kutosha. Pia
akamuamuru rubani azime taa zote ndani ya ndege
ili kuepusha wadunguaji (snipers) wa FBI kufanya
yao.c
Baada ya ndege kusimama mtumishi mmoja wa
kampuni ya Northwest Orient Airlines aliyejulikana
kama Al Lee akiwa amevalia kiraia ili kuepuka
kumchanganya cooper asidhani ni askari akiwa
amevaa sare za uwanja wa ndege, alikabidhiwa
mabegi yaliyokuwa na fedha pamoja na
maparashuti.
Al Lee akaisogelea ndege na Cooper akamuamuru
muhudumu mwingine ndani ya ndege binti aliyeitwa
Mucklow afungue mlango mdogo wa dharura
pembeni ya ndege na kupokea mabegi hayo. Na
Mucklow akatii.
Baada ya Cooper kuhakikisha kuwa fedha na kila
kitu alichohitaji kiko sawa sawa akawaruhusu abiria
wote washuke. Pamoja na abiria alimruhusu
muhudumu Schaffner pamoja na muhudumu
mwingine ambaye alikuwa anaonekana kuwa na umri
mkubwa. Lakini akabaki na marubani wote wawili,
yule binti mwingine muhudumu aliyeitwa Macklow
pamoja na fundi wa ndege.
Kisha akaamuru gari la kujaza mafuta liletwe na
kuwajazia mafuta.
Wakiwa wanawajazia mafuta Cooper aliwapa maagizo
marubani kuhusu anakotaka waende na jinsi
ambavyo anataka wasafiri. Kwanza akawaeleza kuwa
anataka wafuate njia inayoelekea Mexico City na
ndege iendeshe katika speed ya km 190/hour na
ndege iruke umbali wa futi 10,000 kutoka ardhini.
Pia aliwaeleza kuwa anataka waondoe mgandamizo
ndani ya ndege (cabin pressure) na wakiruka
matairi yabaki kana kwamba wanatua, pia mlango
wa nyuma ya ndege ubakie wazi kana kwamba mizigo
inapakiwa na mabawa ya ndege ya pembeni yawekwe
kwenye nyuzi 15.
Baada ya majadiliano kampuni ya Northwest Orient
wakakataa ombi la cooper ndege iruke ikiwa
imefunguliwa mlango wa nyuma mkiani au pembeni
kwa madai kuwa itahatarisha usalama lakini Cooper
kwa kujiamini kabisa akawaeleza kuwa ni salama na
hakutaka kubishana nao sana kwani baada ya ndege
kuruka tu aliufungua mlango wa pembeni
mwenyewe.
Ndege iliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa
Seattle mnamo majira ya saa kumi na moja dakika
arobaini ikiwa na watu watank pekee, yaani Cooper,
muhudumu Macklow, fundi na marubani wawili! Watu
watatu yaani fundi na marubani wawili walikuwa
mbele kabisa kwenye chemba/chumba cha marubani
kuendeshea ndege (cockpit) na Cooper pekee na
muhudumu Macklow walokuwa kwenye sehemu ya
abiria.
Mara tu baada ya ndege kuruka, ndege mbili za
kivita aina ya F-106 kutoka kituo cha kijeshi cha
McChord Air Force Base nazo ziliruka kuifuatilia
ndege iliyotekwa na Cooper na ziliruka katika
namna ambayo zisingeweza kuonekana na Cooper au
mtu yeyote aliyeko ndani ya ndege, ndege moja ya
iliruka juu nyingine chini ya ndege ya akina Cooper.
Baada ya mda kidogo kupita Cooper ali muamuru
muhudumu aende mbele kwenye chumba cha
marubani na akamfungia huko pamoja na wengine
na akabaki peke yake katika sehemu ya kukaa
abiria.
Takribani saa mbili kamili usiku alarm ikalia mbele
kwenye chumba cha marubani kuashiria kuwa kifaa
cha kufungua mlango wa nyuma kwenye mkia wa
ndege kimehuishwa (activated). Dakika chache
baadae sehemu ya nyuma ya ndege ilitikisika kwa
nguvu na kuwa kama inainuliwa juu na marubaini
wakabaini kuwa mlango wa nyuma kwenye mkia wa
ndege ulikuwa umefunguliwa na ili kuepusha ndege
isidondoke marubani iliwalazimu waishushe ndege
chini na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Reno,
Nevada takribani majira ya saa nne na robo usiku.
Baada ya ndege kutua tu maofisa wa FBI na polisi
waliizunguka na kuingia ndani kufanya upekuzi na
ndani ya dakika chache wakagundua D.B Cooper
hakuwepo ndani ya ndege.
MSAKO WA KIHISTORIA.
Baada ya FBI kujiridhisha kuwa Cooper hakuwa
ndani ya ndege nadharia pekee iliyobakia ni kuwa
aliruka ndege ikiwa angani kwani baada ya kuipekua
ndege walikuta paradhuti mbili hazipo. Jambo la
ajabu ni kuwa marubani wa ndege za kivita
zilizokuwa zinaifuatilia ndege ya akina Cooper
walisema kuwa hawakuona mtu akiruka kutoka
kwenye ndege wala parashuti kufunguliwa.
Baada ya kutafakari kwa kina FBI wakaamua
waitengeneza upya safari kama ile ile ambayo
ilitokea siku ya tukio.
Hivyo basi kwa kutumia ndege ile ile na rubani yule
yule FBI walorusha ndege kutoka uwanja wa Seattle
kuelekea uwanja wa Rona, ndege ikiondoka Seattle
muda unaofanana kabisa na ule ambao siku ile ya
utekaji ndege iliondoka Cooper akiwemo ndani.
Kitendawili kikubwa ni mahali gani hasa ndipo
kulikuwa na uwekano kuwa Cooper alitua ardhini.
Lakini ili waweze kujua ni wapi alitua ilikuwa ni
lazima wajua ni mahali gani ndege ikiwa angani
aliruka na kufungua parashuti.
Na kitendawili kingine kama ikitokea wakagundua ni
mahali gani angani ambapo aliruka itawapasa
kung'amua ni muda gani Cooper alitumia kuwa
katika 'mdondoko huru' (free fall) kabla
hajafungua parashuti! Kwasabu mda mrukaji
anaotumia kuwa katika free fall kabla hajafungua
parashuti 'inadetermine' mahali anapotua ardhini.
Kwahiyo baada ya FBI kurusha ndege kutoka uwanja
wa Seattle kuelekea uwanja wa Rona. Kwa
kuzingatia maelezo waliyoyapata kuwa ndege
ilitikisika majira ya saa mbili dakika kumi na tatu
hivyo basi FBI wakafikia muafaka kuwa huo ndio
muda ambao Cooper alifungua mlango wa nyuma ya
mkia wa ndege na kuruka! Kwahiyo FBI nao
wakarusha maafisa kadhaa katika usawa ule ule wa
anga na walibakia katika free fall tofauti tofauti
kabla hawajafungua maparashuti! Baada ya
maafisa wote kutua wakatafuta mzingo
(circumference) wa eneo hilo ambalo ndio eneo
pekee lililokuwa na uwezekano wa Cooper kutua siku
aliporuka.
Na baada ya kubaini ili eneo ambalo Cooper alitua,
walibaini pia kuwa siku ya tukio eneo hili lilikuwa na
mvua kali na kimbunga! Hivyo basi ukizingatia kuwa
Cooper aliruka ndege ikiwa umbali wa futi 10,000
kutoka ardhini na siku ilikuwa na mvua kubwa
iliyoambatana na kimbu na pia ilikuwa ni usiku wa
giza totoro wakakubaliana kuwa hakukuwa na
uwezekano wa Cooper kutua akiwa hai.
Pia walizingatia sababu nyingine kuwa kumbuka siku
ya tukio Cooper aliletewa maparashuti ya kijeshi
alafu akayakataa akadai apewe parushuti nne za
kawaida na FBI wakenda kwenye kituo cha
kufundisha skydiving na wakampatia. Sasa kwenye
yale maparashuti manne, mawili yalikuwa kwa ajili
ya kufundishia tu darasani na mawili ndio yalikuwa
hasa yanaweza kutumika kuruka angani.
Kitu cha ajabu ni kwamba FBI wlikuja kugundua
kuwa Cooper aliyaacha yale maparashuti mawili
ambayo ndio yanayopaswa kutumia kurukia na na
akaruka na yale mawili ya kufundishia darsani
ambapo parashuti moja walidhani kuwa alivaa yeye
na lingine alifunga begi la fedha.
Cont..
0 Comments