sehem ya 3:Coper alivyowasumbua askari

Tuendelee....
Kwahiyo kama ilivyoelezwa awali kuwa siku hiyo
ilikuwa na mvua kubwa na kimbunga kwahiyo FBI
waliamini kuwa maparashuti hayo ya kufundishia
yasingeweza kuhimili hali ya hewa ya siku hiyo na
kumuwezesha Cooper kutua salama, hivyo walifanya
kazi wakiwa na hisia kuwa Cooper hakutua salama.
Baada ya kubaini eneo ambalo ndilo lilikuwa na
uwezekano mkubwa wa Cooper kutua, eneo ambalo
lilikuwa nyikani kuzunguka mto Lewis karibu na ziwa
Merwin! FBI kwa kutumia maofisa waliokuwa kwa
miguu ardhini na helicopters angani wakafanya kazi
ya kulikagua eneo lote hilo.
Lakini pia FBI wakatumia ndege na helicopters
kukagua njia inayopitwa na ndege kutoka Seattle
kwenda Rona (vector 23). Baada ya msako na
upekuzi wa eneo lote hilo kwa siku kadhaa FBI
hawakufanikiwa kumpata Cooper hai au amekufa,
hakupata hata mabaki ya vifaa vya parashuti wala
mabegi.
Pia walitumia submarine kutafuta chini ya sakafu
ya Mto Lewis na Ziwa Merwin lakini kote hakukuwa
na dalili ya Cooper wala mabaki ya vifaa alivyoruka
navyo.
Baada ya mwaka mzima 1971 kuisha pasipo
mafanikio yoyote ya kumpata kupa hai au mwili
wake au hata mabaki ya vifaa alivyoruka navyo FBI
ikabidi iombe msaada kutoka jeshi la marekani
kusaidia msako huo. Hivyo basi jeshi la marekani
wakatoa wanajeshi 200 kusaidia msako huo, pia
wakapata msaada kutoka jeshi la Anga (Air force),
pamoja na wanajeshi kutoka jeshi la ulinzi wa ndani
ya nchi (national guard troops).
Kwa pamoja wakafanya msako wa kina zaidi katika
eneo lote ambalo lilidhaniwa kuwa kuna uwezekano
Cooper ndipo alipotua. Pia kampuni ya EEC ambayo
inahusika na kufukua vitu vilivyozama majini (marine
salvage firm), ilijitolea submarine ili kufanya msako
chini ya ziwa Merwin kuona kama labda yeye Cooper
au vitu alivyoruka navyo alizama umo Msako huu wa
kina uliohusisha maafisa wa FBI, jeshi la marekani,
makampuni binafsi pamoja na national guard troops
ulifanyika kwa siku kumi na nane ndani ya mwezi
march mwaka 1972 na pia ukafanyika tena mwezi
April 1972 kwa siku kumi na nane nyingine.
Msako ulikuwa wa kina hasa kwani nukta baada ya
nukta ilikaguliwa kwenye eneo lote ambalo walihisi
cooper labda ametua ardhini na majini lakini mpaka
msako huu unaisha ndani miezi miwili hiyo
hawakufanikiwa kupata hata unywele au kipande
cha nyuzi ya nguo ya Cooper au mabaki ya kitu
chochote ambacho aliruka nacho siku ya tukio.
Kitendawili kikawa kigumu zaidi. Baada ya misako
mingine mirefu zaidi bila mafanikio FBI ikawabidi
waje na nadharia nyingine kwamba labda walikuwa
wanafanya msako sehemu ambayo sio sahihi. Safari
hii ikawabidi wafanye mahesabu ya kisayansi kabisa
kwa kuzingatia kasi ya upepo siku ya tukio na uzito
wa Cooper na mizigo aliyokuwa nayo na matokeo ya
nadharia yao mpya ya mahesabu ya kisayansi
ikawaambia Cooper atakuwa alidondokea eneo la
kusini mashariki ya eneo walilokuwa wanafanya
msako sasa. Eneo hili jipya walilolibaini kwa
kuongozwa na hesabu za kisayansi lilikuwa
linazunguka mto Washougul.
Hapa napo msako mkali ukafanyika kwa miezi
kadhaa bila mafanikio yoyote.
Baada ya FBI kuona kuwa hakuna mafanikio yoyote
katika misako yao ya maeneo ambayo walidhani
labda cooper alitua ikawabidi wabadilishe nadharia
yote. Sasa wakaweka nadharia mpya kuwa labda
kuna uwezekano Cooper alitua salama salimini na
yuko mtaani anatumbua hela zake.
Hivyo basi kwa kuwa FBI walizipiga picha noti moja
moja ya fedha zote alizopewa Cooper (kumbuka
walimpa noti 10,000 za dola 20). Kwahiyo walikuwa
na serial number ya kila noti aliyopewa Cooper. FBI
wakasambaza serial number hizi kwenye mabenki,
macasino, maduka na kila sehemu ambayo fedha
inatumika lengo ni kuwa kama noti hata moja
ambayo Cooper alipewa itatumiaka mahali popote na
kuingia kwenye mzunguko wa hela basi FBI
watadetect na kutrace hiyo hela imetoka kwa nani.
Lakini wakasubiri miezi na miaka hakuna noti hata
moja ambayo iliingia kwenye mzunguko wa hela.
Kitendawili kikazidi kuwa kikubwa zaidi! Kama
Cooper hakufanikiwa kutua salama kwanini
wameshindwa kupata mwili wake au mabaki ya vitu
alivyoruka navyo ukizingatia kuwa wamefanya msako
nukta baada ya nukta ya sehemu ambayo alitua. Na
kama alitua salama na kuingia mtaani, kwanini
hazitumii hela alizozipata maana hakuna noti hata
moja kwenye mzunguko.
Fumbo hili liliwatesa FBI kwa miaka saba mpaka
mwaka 1978 ambapo mwanga kidogo ulipatikana
kuhusu tukio hili..
VIDHIBITI VINAFANYA FUMBO KUWA GUMU ZAIDI
BADALA YA KUSAIDIA
Mwaka 1978 muwindaji mmoja aliokota kikaratasi
chenye maelekezo ya namna ya kushusha mlango wa
nyuma wa ndege aina ya Boeing 737 (Northwest
Orient Flight 305 ilikuwa ni Boeing 727) na FBI
wanaamini labda kikaratasi hiki kilidondoshwa na
Cooper.. Lakini kidhibiti hiki hakikusaidia sana.
Kidhibiti ambacho kilikuwa na mchango mkubwa
kwenye kuleta maswali zaidi kwa FBI kilipatikana
mwaka 1980.
Mtoto wa miaka 8 aliyeitwa Brian Igram akiwa
kwenye vacation na familia yake kwenye beach ya
mto Columbia alikuwa akichimba chini ili kusaidia
familia kuwasha moto waote. Igram alikuwa
akichimba kwa mikono kama watoto wafanyavyo na
akachimba shimo refu kiasi na akiwa anachimba
alikutana na makaratasi. Baada ya kuyatoa hayo
makaratasi kutoka kwenye shimo alilochimba wazazi
wake waligundua kuwa zilikuwa na vibunda vitatu
vya hela.
Baada ya kuzichunguza kwa makini wazazi wakahisi
kuwa inawezekana fedha hizo zinahusiana na D.B
Cooper tukio ambalo lilitawala kwenye vyombo vya
habari kwa kipindi hicho. Hivyo basi wazazi
wakawasiliana na vyombo vya ulinzi na baada ya FBI
kuzisoma serial number za noti hizo wakathibitisha
kuwa ni kweli noti hizo ni sehemu ya fedha
alizopewa D.B Cooper mwaka 1971. Swali, je
zilifikaje pale?
Hivyo basi FBI ikatumia wataalamu wake ili kupata
mwanga kidogo.
Kwanza vibunda vyenyewe vya hela vilikuwa kama
ifuatavyo; kila kibunda kilikuwa peke yake
kinajitegemea kimoja kilikuwa na noti 100
zilizofungwa pamoja kwa rubber band isipokuwa
kibunda kimoja tu ambacho kikikuwa na noti 90
lakini nazo zilifungwa pamoja kwa rubber band.
Pia licha ya kuwa noti zilikuwa zimefungwa pamoja
kwa rubber band lakini zilikuwa zimekaa hovyo hovyo
katika umbo la mviringo na wataalamu wa FBI
wakatoa conclusion kwamba zilikuwa zimekaa hovyo
hivyo kwa umbo mviringo kwasababu zilikuwa zime
'kururuka' na maji ya mto kutoka mahali fulani na
kuna kunasa hapo.
Na hakika huu ndio ufafanuzi ambao angalau
ulikuwa unaingia akilini.
Lakini swali linakuja; inawezekanaje vibunda vitatu
vya hela ambavyo havijaungana kila kimoja
kinajitegemea 'vikururuke' na maji alafu vije vyote
vinase sehemu moja? Kitu kama hicho ni almost
imposible.
Kutokana na kesi hii kuteka vyombo vya habari
kipindi hicho kugundulika kwa noti hizi kuliteka hisia
za watu na hii ikapelekea mtaalamu wa jiolojia
aliyeitwa Leonard Palmer kutoka chuo kikuu cha
Portland kufanya tafiti katika beach ambayo
vibunda hivi vitatu vilipatikana na matokeo ya
utafiti wake ndio yalishangaza zaidi FBI.
Kwanza kabisa kumbukumbu zilionyesha kuwa
sehemu kubwa ya mto Columbia ikiwemo sehemu
vinunda hivi vya hela vilipatikana ilifanyiwa
dredging mwaka 1974. Dredging ni vile wanatumia
vifaa maalum kutoa udongo chini ya mto na
pembezoni mwa mto na kuumwaga kwenye beach ya
mto. Kitendo hiki huwa kinafanyika ili kuongeza
kingo za mto au kuboresha ubora wa beach.
Sasa basi, alichokigundua huyu mtaalamu ni kwamba
katika lile shimo ambalo mtoto Igram alichimba na
kukuta vinunda vya hela za Cooper chini yake
kulikuwa na matabaka mawili ya udongo na
ukichimba tena unakutana na tabaka la tatu ambalo
lina udongo wa mfinyanzi ambao ndio udongo
unaopatikana baada ya kufanya dredging. Sasa hii
ina maana gani? Maana yake ni kwamba hivyo
vibunda vya hela za Cooper vilikuwa deposited hapo
baada ya dredging kuwa imeshafanyika. Sasa
kumbuka kuwa dredging ilifanyika mwaka 1974 na
tukio la Cooper likitokea mwaka 1971.
Kuna tofauti ya miaka miatatu hapo. Sasa je hivi
kweli inawezekana hela zikururuke na maji miaka
mitatu na kwa bahati mbaya au nzuri isiyomithilika
bibunda vitatu vyote vikwame sehemu moja?
Kama hiyo haitoshi; kumbuka kuwa mtaalamu
anasema kuwa chini ya shimo alilochimba mtoto
Igram kulikuwa na matabaka mawili ya udongo ndipo
ufikie tabaka la udongo mfinyanzi uliotokana na
dredging hii inamaanisha kuwa baada ya dredging
kufanyika mwaka 1974 ilipita miaka kadhaa
amabapo yale matabaka mawili mengine
yakajitengeneza kwa juu ya udongo mfinyanzi ndio
hivyo vibunda vya hela za Cooper zikawa deposited
hapo.
Na mtaalmu alikisia hivyo vibunda vya hela
vimekuwa deposited hapo labda miaka miwili tu
iliyopita. Sasa huo ulikuwa ni mwaka 1980, miaka
miwili nyuma maana yake ni 1978 na kumbuka tukio
la Cooper lilitokea mwaka 1971.! Kuna tofauti ya
miaka saba hapo katikati. Na hili lilikuja kuungwa
mkono na kikosi kazi maalum kilichoundwa baadae
na FBI kilichojulikana kama Cooper Research Team
kuwa vibunda vya hela lazima vilikuwa deposited
hapo miaka kadhaa baada ya tukio la sivyo rubber
band walizozikuta vimeshikilia noti zingekuwa
zimeharibika kabisa.
Ugunduzi huu uliwapa maswali na kuwachanganya
zaidi FBI badala ya kuwasaidia kwasababu haiingii
akilini hela zikururuke na maji miaka saba.
Kumbuka umbali kutoka mto Columbia na 'Vector
23' (njia ambayo ilipita ndege ya akina Cooper siku
ya tukio) kulikuwa na umbali wa kilometa 20.
Hivyo basi hata kama maji yangekuwa yanatembea
taratibu isingechukua zaidi ya dakika 40 kwa
vibunda hivyo kufika hapo. Kwahiyo kwa namna
yoyote ile isingewezekana kwa sehemu ya kuchukua
dakika 40 itumike miaka saba, na kwa namna yeyote
ile habadani haiwezekani vibunda vitatu ambavyo
havijashikana vije vikwane exactly sehemj moja!
Katika ofisi ya FBI maswali na mafumbo yalikuwa
mengi kuliko majibu! Hizo fedha za Cooper
zimefikaje pale? Zimekuja na maji? Mtu kaziweka?
Kama ni mtu kwanini aziweke pale? Je, fedha
nyingine ziko wapi? Kwnini vibunda viwili vina noti
100 kila kimoja na kibunda kimoja kina noti 90 tu?
Noti kumi zimeenda wapi? Na hii inatoa clue gani
kuhusu D.B Cooper?
Baada ya miaka sita ya kitendawili kuhusu fedha
zilizookotwa zimetoka wapi hatimaye mwaka 1986
FBI ikanyoosha mikono juu na kusalimu amri kuwa
fedha hizo zilizookotwa haziwezi kuwasaidia kumpata
Cooper. Hivyo basi wakafikia makubaliano ya
kuziganya fedha. FBI wenyewe wakachukia noti 14
kama kidhibiti na noti zilizobaki zikagawanywa kwa
kijana Igram aliyeziokota na nyingine wakapewa
kampuni ya Bima waliowalipa fidia Northwest Orient
Airlines.
Igram aliziuza kiasi kidogo cha baadhi ya noti zake
mwaka 2008 katika mnada wa hadhara kwa thamani
ya Dola 37,000.
Mpaka leo hii noti nyingine zilizobakia ambazo
Cooper alipewa mwaka 1971 (takribani noti elfu tisa
na mia saba) hazijulikani zilipo.
Tutaendelea Kesho.... GoodNight Guys...

Post a Comment

0 Comments