Sumu lyrics by Fid q



Alieniumba alinipa mdomo hovyo nina haki ya
kuongea/ ni bahati nimeotea..safi… Kamwe siachi
kuishea/ hamtaki niwe fair…? Trust me.. Me huwa
happy niki-care/ na ninaowatouch husema” mshkaji
upo smart upstairs / usiache kuongea/ usiache
wewe ni incharge huna spear/ kipaji ka ngwear/kwa
mpaji ni ka zawadi aliwagea/flag pepea/alihitaji
zaidi ya Maji na mmea…? Ilikuaje wamuache hadi
mshkaji ulaji wa drags ukamzoea ..?
Tunamoka ili kusafiri kihisia au kufoka pia…ikotoka
ukaisikia..huwezi ichoka au kuotosa ikikuingia../
kinachoichosha hii nia…ni kulosa ulichokiota
kupatia..kiwachota kihisia…tunasota je inatosha hii
fidia..?
Shibe ya mdau hainilazi njaa, sababu mganga yupo
juu../ furaha ya baadhi ya wadau ni kuona star
anawalamba miguu.
Asie nihitaji simuhitaji, kamwe simuachi anijazie
INZI../ bandidu kama TSOTSI sipigi goti kama
PNC../ hakuna  ambae hakosi labda ZIZI kwa DEE
ANDY../ yangu self esteem haitoki ka riport za
TMZ
Na hainizuii nisile mkate kwa kuhofia..kiungulia…/na
uemcee hauniachi huniangalia ka fidelia../ka bruce
lee hizi karate mtatupigia.. Mtaishia…/na sintosita
kusema asante kwa kunisaidia au kuwasifia .. Kwa
kunisaidia…
Washkaji baadhi hawana haki ya kuipresha hii
medula…/wao wako radhi kukupa pombe na si pesa
ya kula….
Nawaona vyura tu kama snura hii sura ya muhuni
haina gere…/ mastar wanaovaa masut mtaani
nyumbani kunguni tele…
Kwa magonjwa yanayotibika tunapoteza maisha..
Huruma../watachanga kwenye msiba ukifa..
Hawajali ukiumwa..
Au wanaweza wakahisi umekufa kwa kukutwa
umezirai…/ usipo stuka Africa unaweza kuzikwa
ukiwa hai…
Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji../
ukinizuga kwa ulaji takupa fact kwa lugha ya
kiushkaji…
Mnataka vitu rahis..? Me nawapa vitu halis…/
watata mnamtaka ibilisi../na sio huyu big kaka ka
idris…
Mrnice jua lanutosi na mtaa unakiu ile mbaya…/
hawamsaport isipokuwa wanawapromoti
aliowainspaya…
Wakati ney sio kama moxie STOSHI hakupaswa
kumgwaya../ lakini uzee bila noti ni zaidi ya nyoshi
akiwa vibaya….
I didn’t come this far just to come this far…/
siwezi sanda kama bikra hata nikiishi kistar
Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unacho
tafta…/ pesa ya sadaka wazushi wanaivuta kwa
chafu tatu….
Binadam wako wapi hadimnanitoa mie nisiwemo.. /
leo nawapa offer ya mswaki halafu kesho
mnaning’oa meno..?
Time is money, nafasi haijali kukuzuga../ Wema
anataka saa ya almasi ZARI anaujali muda..
Washa sana nyasi, raster yupo kwa fasi vuta../
wanashindwa kujinafas kwa unafki nafsi
zinawasuta…
Wabongo wa majuu hamna upendo mnajigawa../
Uongo hauna miguu lakini skendo zinamabawa…
Aliemtia umaskini Africa leo analia kwa
yanayomsibu…/ na humtangaza akimpa msaada kiasi
cha kumtia aibu…
Dunia sio chafu.. Ni chafu.. Uchafu tukiutazama../
kuna sumu ndani ya watu na hapo hapo
tunapokwama…
Hawaamini kwenye kuunda Diamond au KIBA
wawili../ wanachoamini ni kumshusha mmoja ili
mmoja awe dili…
Cha kupewa hakishibishi.. Ukipewa lazima
ukumbushwe…/ Dunia mwendo wa ngisi kung’aa sio
lazima star ashushwe..
Ukiacha hisia zikuendeshe Kwa ujeuri utaishia
kufeli../ neno la kweli sio zuri na  zuri halina
ukweli…
Nitasahau vyote.. Lakini milele tamkumbuka alie
niumba../ na daily takaa mkao wa push-up tu
kama Umbwa

Post a Comment

0 Comments