TUKIO LA KWELI KATIKA MAISHA HALISI.
Siku ya November 24 mwaka 1971, katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa mji wa Portland jamaa
aliyevaa suti nyeusi na koti refu jeusi kwa juu akiwa
amebeba brief case nyeusi alifika katika counter ya
kampuni ya ndege ya Northwest Orient Airlines na
akatoa fedha cash dola 20 kununua tiketi ya ndege
Flight 305 kwenda mjini Seattle, ambayo kwa
kawaida ni safari inayochukua dakika 30. Jamaa
huyu alijitambulisha kama 'Dan Cooper'.
Baada ya kuingia kwenye ndege akakaa kwenye siti
namba 18C, baadae akakaa siti namba 18E na
baadae 15D.
Ilipofika mida ya saa nane na dakika hamsini
mchana ndege ikaruka na baada ya ndege kuruka
Mr. Cooper akawasha sigara na akaagiza soda!
Siti ambayo alikaa Cooper ilikuwa siti ya nyuma
kabisa na alikaa karibu kabisa na siti ya muhudumu
wa ndege wa kike aliyeitwa Florence Schaffner.
Baada ya dakika chache Cooper alitoa kikaratasi
mfukoni kilichochapwa kwa unadhifu na maandishi
yakiwa yameandikwa kwa herufi kubwa na kisha
akampatia Bi. Schaffner kikaratasi hicho.
Baada ya Bi. Schaffner kupokea kikaratasi,
kutokana na mazoea akajua ni kawaida tu abiria
alikuwa ametokea kumtamani na hivyo amempa
namba ya simu, kwa hiyo Bi. Schaffner hakukisoma
kikaratasi bali alikiweka moja kwa moja kwenye
mkoba. Mara baada ya kukiweka kikaratasi kwenye
mkoba, Cooper akainama kidogo na kumnong'oneza
Bi. Schaffner na kumwambia "Miss you would
better take a look at that note. I have a bomb
" (Bibie ni vyema ungekisoma hicho kikaratasi. Nina
bomu).
Baada ya kumueleza hivyo kimya kimya
akamuamuru muhudumu huyo akae karibu nae na
kuanza kumpa maagizo. Lakini kabla ya hapo yule
mhudumu akataka ampe uhakika kama kweli ana
bomu. Cooper akachukua briefcase yake na
kuifungua kidogo tu ili muhudumu aangalie na
alipoangalia ndani ya briefcase akaona cylinders
nane, nne zikiwa chini na nne zikiwa juu zikiwa
zimeunganishwa kwa nyaya nyekundu ambazo nazo
zinaenda kuunganika kwenye battery yenye rangi
nyekundu pia ikiyopo pembezoni mwa briefcase.
Baada ya kuchungulia muhudumu akaamini kweli
Cooper alikuwa na Bomu.
Cooper akampa maagizo muhudumu akaongee na
marubani kwa kupitia intercom kuwa wawasiliane na
uwanja wa ndege wa Seattle na wawaeleze juu ya
ndege kutekwa na mtu mwenye bomu na yuko
tayari kulipua ndege hiyo na abiria wote 36 na
watumishi wa ndege 6 waliopo umo ndani.. (Ndege
ilikuwa haijajaa yote, ilijaa kama theluthi moja tu
(1/3)).
Ili asilipue ndege hiyo Cooper alihitaji apewe 'Fedha
halali za kimarekani' dola 200,000 (msemo huu
'fedha halali za kimarekani' utakuja kuleta maana
sana huko mbele kwenye upelelzi wa FBI). Pia
aliamuru apewe parashuti nne na ndege itakapofika
uwanja wa ndege wa Seattle kuwe na gari ya kujaza
mafuta inasubiri ili ijaze ndege mafuta na
kumpeleka sehemu atayoitaka.
Muhudumu Bi. Schaffner akawasiliana na mapilot na
kuwahakikishia kuwa ni kweli jamaa ana bomu na
akawapa orodha ya vitu alivyokuwa anavitaka.
Baada ya kupewa orodha ya demands za Bwana
Cooper, marubani wakawasiliana na uwanja wa
ndege wa Seattle na watu wa uwanja wa ndege
wakawasiliana na vyombo vya ulinzi na baada ya
mtiririko wa mawasiliano kati ya uwanja wa ndege,
wamiliki wa ndege na vyombo vya ulinzi kufanyika
wakakubaliana kuwa ili kuepusha hasara ya
kibiashara na kupoteza maisha ya watu 42 ni vyema
wakampatia mtekaji anavyovitaka lakini vyombo vya
ulinzi vitaangalia kama kutapatikana fursa yoyote
waweze kumkata au kumdungua mtekaji huyo.
Hivyo basi wahudumu wote waliopo kwenye ndege
waliamuliwa wampe ushiriakiano Cooper ili kuepusha
hatari yoyote na pia wamueleze kuwa awape mda
kidogo ili kukamilisha kupata vitu alivyokuwa
anavihitaji.
Baada ya jibu hilo kurudishwa juu kwenye ndege na
marubani kuwasiliana na muhudumu Schaffner
kupitia intercom, muhudumu alirudi kwenye siti
aliyokaa Cooper na alikuta sasa amevaa miwani
meusi ya jua na yuko amerelax kabisa bila presha
wala wasiwasi wowote! Akampatia jibu walilopewa
kutoka chini kwenye uwanja wa ndege.
Cont...
0 Comments